Mar 13, 2018 15:41 UTC
  • Mkutano wa Miujiza ya Kisayansi wa Qur'ani waanza Misri

Mkutano wa Kumi wa Muujiza wa Kisayansi katika Qur'ani na Suna umeanza katika Chuo Kikuu cha Mansoura kilichoko umbali wa kilomita 120 kaskazini mashariki mwa mji wa Cairo nchini Misri.

Mwenyekiti wa mkutano huo, Mujahid Abul Majd amesema kuwa, lengo kuu la mkutano huo ni kuonesha mfungamano mkubwa uliopo baina ya dini ya Uislamu na sayansi na elimu. 

Ameongeza kuwa, dini ya Uislamu daima inawaita wanadamu katika elimu na uvumbuzi.

Wakati huo huo Dokta Abdullah Baothman ambaye ni Mshauri wa Katibu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kitabu na Suna amebainisha muujiza wa kisayansi wa Qur'ani na Suna na kusema kuwa, Qur'ani tukufu na Suna za Mtume (saw) zinawataka wanadamu kutadabari na kutafakari kwa kina katika uwezo na qudra ya Mwenyezi Mungu na viumbe vyake. 

Mkutano huo wa siku tatu ulioanza jana unajadili muujiza wa Qur'ani mkabala wa ukafiri.

Makala 16 za wajumbe wa jumuiya za vyuo vikuu, vituo vya utafiti na madaktari zimewasilishwa katika mkutano huo. 

Tags