Raia wa Afghanistan waandamana kulaani mauaji ya Marekani dhidi yao
https://parstoday.ir/sw/news/world-i42668-raia_wa_afghanistan_waandamana_kulaani_mauaji_ya_marekani_dhidi_yao
Raia wa mji wa Kunduz, kaskazini mwa Afghanistan wamefanya maandamano makubwa kulaani jinai za kila mara zinazofanywa na ndege za kijeshi za askari wa kigeni wakiongozwa na Marekani, katika maeneo tofauti ya nchi yao.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 05, 2018 02:53 UTC
  • Raia wa Afghanistan waandamana kulaani mauaji ya Marekani dhidi yao

Raia wa mji wa Kunduz, kaskazini mwa Afghanistan wamefanya maandamano makubwa kulaani jinai za kila mara zinazofanywa na ndege za kijeshi za askari wa kigeni wakiongozwa na Marekani, katika maeneo tofauti ya nchi yao.

Washiriki wa maandamano hayo yaliyofanyika katika eneo la Dasht-e-Archi la mji huo, sambamba na kulaani vikali mashambulizi ya anga ya askari hao vamizi, wametaka kukomeshwa mara moja jinai hizo. Kadhalika waandamanaji wameitaka serikali ya Kabul kufuatilia suala hilo haraka. Wakati huo huo, wawakilishi kadhaa wa bunge la Afghanistan wamelaani vikali mashambulizi hayo ya askari wa kigeni kupitia kikao cha Jumatano ya jana ambapo walizitaja jinai hizo kuwa ni mauaji dhidi ya Waislamu.

Moja ya jinai za askari katili wa Marekani nchini Afghanistan

Inafaa kuashiria kuwa, katika shambulizi la anga la askari hao siku ya Jumatatu ndani ya eneo la Dasht-e-Archi la mji wa Kunduz, makumi ya raia waliuawa wakiwemo watoto wadogo. Jumla ya askari wa kigeni elfu 19 wakiwemo askari elfu 16 wa Marekani, wako nchini Afghanistan kwa kisingizio cha kupambana na makundi ya kigaidi na kuzuia madawa ya kulevya.

Waafghani wakiandamana kwa hasira

Hii ni katika hali ambayo raia wa Afghanistan wanaamini kwamba, uwepo wa askari wa kigeni nchini mwao tangu mwaka 2001, haujasaidia hata kidogo kudumisha amani na kinyume chake, umehusika kuongezeka makundi ya kigaidi na uzalishaji mihadarati. Kadhalika askari hao wanamekuwa wakifanya mauaji ya kila mara dhidi ya raia wa kawaida kila uchao ndani ya taifa hilo.