Korea ya Kaskazini yakadhibisha madai ya Marekani
Ofisi ya Uwakilishi ya Korea ya Kaskazini katika Umoja wa Mataifa imekadhibisha tuhuama za Marekani dhidi ya Pyong Yang kuhusu kuhakiwa vituo vya taarifa vya kamati za vikwazo za Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Ofisi ya Uwakilishi ya Korea ya Kaskazini katika Umoja wa Mataifa leo imetoa ripoti na kueleza kuwa Marekani imetoa tuhuma hizo ili kulinda anga ya vikwazo na kuendeleza mashinikizo dhidi ya Korea ya Kaskazini kwa gharama yoyote ile; tuhuma ambazo hazina hadhi ya kuchunguzwa.
Taarifa ya Korea ya Kaskazini imeongeza kuwa Marekani na nchi nyingine adui ni vyema kuelekeza juhudi zao katika kumaliza mivutano na kurejesha amani katika Peninsula ya Korea badala ya kuendesha njama na kuzusha tuhuma zisizo na msingi kwamba Korea ya Kaskazini imehusika na udukuzi huo wa taarifa.
Ofisi ya Uwakilishi ya Korea ya Kaskazini imetoa taarifa hiyo kabla ya kufanyika kikao kati ya Kim Jong un Kiongozi wa Korea ya Kaskazini na Rais Donald Trump wa Marekani mwezi Mei au mwanzoni mwa mwezi Juni mwaka huu.