May 20, 2018 14:34 UTC
  • Marekani wazidi kutwangana risasi, 156 wauawa na kujeruhiwa masaa 48 yaliyopita

Kituo cha kukusanya takwimu za mauaji na mashambulizi ya kutumia silaha nchini Marekani kimetangaza habari ya kuuawa na kujeruhiwa watu 156 katika kona mbalimbali za nchi hiyo inayojigamba kuwa na usalama mkubwa katika kipindi cha masaa 48 yaliyopita.

Shirika la habari la IRIB limekinukuu kituo hicho kikitoa ufafanuzi katika ripoti yake ya leo Jumapili kwamba matukio 67 za kupigana risasi yameripotiwa kwenye kipindi cha masaa 24 iliyopita katika majimbo tofauti ya Marekani na watu wasiopungua 21 wameuawa na wengine 48 wamejeruhiwa kwa risasi katika matukio hayo. 

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, matukio mengi zaidi ya kupigana risasi yametokea katika majimbo ya Texas, Illinois, Louisiana na Missouri.

Raia wa Marekani wamechoshwa na mauaji ya kiholela ya silaha

 

Kituo hicho cha kutoa takwimu za mashambulizi ya kutumia silaha nchini Marekani pia kimesema, katika ripoti yake hiyo kwamba katika kipindi cha masaa 48 yaliyopita kumeripotiwa matukio 196 ya kupigana risasa katika miji na majimbo tofauti ya nchi hiyo. Watu 41 wameuawa na wengine 115 kujeruhiwa katika matukio hayo. 

Maelfu ya watu wanauliwa kwa risasi nchini Marekani kila mwaka na matukio hayo yanatokea katika miji na majimbo tofauti ya nchi hiyo, suala ambalo linaonesha kuwa nchi nzima ya Marekani haina usalama; tofauti na propaganda zinazoenezwa kuwa nchi hiyo ni kiranja wa watu kuishi kwa usalama na amani duniani.

Tags