Putin: Hatutaruhusu Marekani ijifanye polisi wa dunia
https://parstoday.ir/sw/news/world-i45554-putin_hatutaruhusu_marekani_ijifanye_polisi_wa_dunia
Rais Vladimir Putin wa Russia amesema, hatua za upande mmoja za rais wa Marekani ndio chanzo hasa cha kuongezeka mivutano duniani.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 08, 2018 00:05 UTC
  • Putin: Hatutaruhusu Marekani ijifanye polisi wa dunia

Rais Vladimir Putin wa Russia amesema, hatua za upande mmoja za rais wa Marekani ndio chanzo hasa cha kuongezeka mivutano duniani.

Putin ameyasema hayo katika mkutano wake wa kila mwaka wa masuali na majibu na waandishi wa habari, ambapo mbali na kutoa indhari kwa hatua za upande mmoja zinazochukuliwa na Marekani duniani amesema, Moscow haitaruhusu Marekani ijifanye polisi wa uchumi wa dunia.

Rais wa Russia ameongeza kuwa mashinikizo yanayotolewa dhidi ya mashirika ya nchi hiyo yanapoteza imani kwa sera za kiuchumi za nchi za Magharibi.

Rais Vladimir Putin wa Russia akisikiliza suali la mmoja wa waandishi wa habari

Katika mkutano wake huo wa masuali na majibu na waandishi wa habari, Putin aidha amesema kuhusu kadhia ya kupewa sumu Sergei Scripal, jasusi wa zamani wa Russia nchini Uingereza kwamba serikali yake inataka kuwasiliana na Yulia Scripal, binti wa jasusi huyo na vilevile kushirikishwa katika uchunguzi wa kadhia hiyo.

Rais wa Russia amesisitiza kwa mara nyingine kuwa baada ya Sergei Scripal na binti yake Yulia watakaporuhusiwa kutoka hospitali, Moscow inataka ipatiwe fursa ya kukutana nao.

Akijibu suali kuhusu tuhuma za Marekani na Ulaya dhidi ya nchi yake, Rais Putin amesema mtazamo wa Magharibi wa kuiandama Russia kwa tuhuma ni makosa na wala hauna msingi na utasababisha madhara kwa pande zote.../