Jul 25, 2018 04:27 UTC
  • Watu 74 wapoteza maisha katika janga la moto nchini Ugiriki

Idadi ya watu waliopoteza maisha nchini Ugiriki baada ya moto mkubwa kuzuka kilomita 35 mashariki mwa mji mkuu Athens imefikia 76.

Taarifa zaidi zinasema kuwa, moto mkubwa uliozuka na kuunguza msitu nchini Ugiriki umeua kwa uchache watu 74, huku mamlaka nchini humo zikisema kuwa, zinahitaji msaada wa kimataifa ili kukabiliana na moto huo ambao ni janga kubwa kuwahi kushuhudiwa kwa zaidi ya muongo mmoja.

Moto mkali unaoshambaa kwa kasi kutokana na upepo mkali umesababisha uharibifu mkubwa katika kijiji kilichoko ufukweni mwa bahari cha Mati, na kuyaharibu magari na nyumba katika eneo hilo.

Waokozi wamepata makuumi ya miili wakiwemo watoto ambao wanaonekana kukumbatiana walipokuwa wanafariki, wakiwa wamekwama katika moto huo uliozuka mita chache chache kutoka baharini.

Wafanyakazi wa zimamoto wakiwa kazini

Mamia ya wafanyakazi wa vikosi vya zima moto, wanaendelea na jitihada za kuuzima moto huo, huku watu wakiwa wameyakimbia makazi yao katika maeneo ya karibu na mji mkuu Athens.

Alexis Tsipras, Waziri Mkuu wa Ugiriki amesema kuwa, watafanya lolote linalowezekana kibinadamu kuhakikisha  kwamba, wanaokoa maisha ya watu. Waziri Mkuu huyo  amelazimika kukatisha ziara yake nchini Bosnia na kurejea nyumbani.

Timu za uokozi zinasema kuwa, wanakabiliwa na hali ngumu katika operesheni ya uokoaji kutokana na ukubwa wa moto huo na hali mbaya ya upepo ambao umekuwa ukiufanya moto huo usambae kwa kasi.

Tags