Foreign Policy: Trump anaupotosha umma kuhusu hali ya umasikini Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i47235-foreign_policy_trump_anaupotosha_umma_kuhusu_hali_ya_umasikini_marekani
Jarida la Foreign Policy limetoa ripoti na kueleza kwamba serikali ya Marekani inaupotosha umma kuhusu hali ya umasikini nchini humo.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Aug 04, 2018 22:02 UTC
  • Foreign Policy: Trump anaupotosha umma kuhusu hali ya umasikini Marekani

Jarida la Foreign Policy limetoa ripoti na kueleza kwamba serikali ya Marekani inaupotosha umma kuhusu hali ya umasikini nchini humo.

Jarida hilo linalochapishwa nchini Marekani limeandika kuwa takwimu za hali ya uchumi zilizotolewa hivi karibuni na Ikulu ya White House kuhusu ukuaji wa uchumi na kupungua kiwango cha umasikini na watu wasio na ajira ni za upotoshaji kwa sababu Shirika la Kimataifa la Umoja wa Mataifa lilitangaza mwezi Mei kwamba kuna masikini milioni 40 nchini Marekani na zaidi ya milioni tano miongoni mwao maisha yao ni ya "hali ya ulimwengu wa tatu."

Ripoti hiyo ya jarida la Foreign Policy imeongeza kuwa takwimu za White House kuhusu kupungua kiwango cha umasikini nchini Marekani ni za utiaji matumaini kupita kiasi na zimetiliwa shaka na wanauchumi na wataalamu wa takwimu.

Mama masikini na watoto wake wasio na pa kuishi

Foreign Policy limebainisha kwamba ripoti iliyotolewa na Umoja wa Mataifa kuhusu uhalisia wa hali ya umasikini ndani ya jamii ya Marekani imeshadidisha mikwaruzano kati ya Washington na umoja huo.

Sera za serikali ya Rais Donald Trump kuhusu mipango ya ustawi wa jamii zimezidisha wasiwasi wa kuongezeka umasikini  na kuzidi kuwa mbaya hali ya raia masikini nchini Marekani.

Mwaka uliopita wa 2017, Trump aliufuta mpango wa bima ya matibabu ya gharama nafuu maarufu kama Obamacare na kusababisha raia milioni 25, wengi wao wakiwa ni watu masikini wapoteze fursa hiyo ya matibabu.../