Amnesty International lakosoa siasa za ubaguzi zinazotekelezwa na Trump
https://parstoday.ir/sw/news/world-i47414-amnesty_international_lakosoa_siasa_za_ubaguzi_zinazotekelezwa_na_trump
Shirika la Msamaha Duniani la Amnesty International na katika kumbukumbu za mwaka mmoja za matukio ya Charlottesville, Marekani limekosoa siasa za ubaguzi zinazotekelezwa na Rais Donald Trump wa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 13, 2018 03:32 UTC
  • Amnesty International lakosoa siasa za ubaguzi zinazotekelezwa na Trump

Shirika la Msamaha Duniani la Amnesty International na katika kumbukumbu za mwaka mmoja za matukio ya Charlottesville, Marekani limekosoa siasa za ubaguzi zinazotekelezwa na Rais Donald Trump wa nchi hiyo.

Margaret Huang, mkuu wa idara ya utendaji ya Amnesty International na katika kumbukumbu ya mapigano yaliyotokea kwenye mji wa Charlottesville amesema kuwa, Trump ameziweka hatarini haki za Wahindi wekundu, wahajiri, wahamiaji na Waislamu. Katika taarifa hiyo imeelezwa kwamba, mwaka jana viongozi wa Marekani na kwa namna ya wazi waliunga mkono hatua za makundi ya kibaguzi katika jimbo la Virginia.

Rais Donald Trump wa Marekani anayeunga mkono makundi ya kibaguzi

Itakumbukwa kuwa, mwaka jana makundi yanayoendesha kampeni za ubaguzi katika mji wa Charlottesville, jimbo la Virginia nchini Marekani yaliwashambulia watu wa kawaida ambapo mtu mmoja aliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa. Takwimu zinaonyesha kwamba, vitendo vya kibaguzi vinavyofanywa na makundi ya mrengo wa kulia , vilishika kasi zaidi tangu alipoingia madarakani Rais Donald Trump. Hii ni kwa kuwa rais huyo anaunga mkono vitendo vya makundi hayo yanayoendesha kampeni za ubaguzi.