Mashambulizi dhidi ya wanawake wa Kiislamu yaongozeka Ubelgiji
(last modified Mon, 10 Sep 2018 04:10:44 GMT )
Sep 10, 2018 04:10 UTC
  • Mashambulizi dhidi ya wanawake wa Kiislamu yaongozeka Ubelgiji

Takwimu zinaonesha kuwa, karibu asilimia 76 ya wanawake Waislamu nchini Ubelgiji walishambuliwa na magenge ya watu wanaopinga Uislamu nchini humo katika mwaka uliopita wa 2017.

Ripoti zinasema kuwa, Jumuiya ya Kimataifa ya Kuzuia Propaganda Chafu dhidi ya Uislamu nchini Ubelgiji imetoa ripoti kuhusu takwimu za mashambulizi yanayofanywa na makundi ya wanaopiga vita Uislamu mwaka 2017 na kutangaza kuwa, shambulizi moja la aina hiyo limekuwa likifanyika nchini Ubelgiji kila baada ya siku mbili.

Ripoti hiyo imesisitiza kuwa, karibu asilimia 29 ya mashambulizi hayo yamefanyika katika mitandao ya kijamii, 17 dhidi ya misikiti na vituo vya masomo vya Waislamu, asilimia 14 dhidi ya maeneo yao ya kazi na asilimia iliyokabia ya mashambulizi hayo yamefanyika dhidi ya wanawake wa Kiislamu katika maeneo mengine nchini humo. 

Waislamu Ulaya wanapinga ubaguzi na machafuko.

Ripoti hiyo imesema kuwa, Wanawake Waislamu wamekuwa wakishambuliwa zaidi kuliko Waislamu wa kiume kutokana na mavazi yao na kwamba washambuliaji wengi ni wanaume. 

Mashambulizi na chuki dhidi ya Uislamu vimeenea sana barani Ulaya katika miaka ya hivi karibuni na vimeshika kasi kubwa zaidi katika nchi za katikati mwa bara hilo ikiwemo nchi ya Ubelgiji.    

Tags