Parnham akiri kuanzisha wimbi la mashambulizi dhidi ya Waislamu Uingereza
https://parstoday.ir/sw/news/world-i48778-parnham_akiri_kuanzisha_wimbi_la_mashambulizi_dhidi_ya_waislamu_uingereza
Mbaguzi mashuhuri wa rangi wa Uingereza amekiri kwamba amekuwa akiwachochea raia wa nchi hiyo kuwashambulia Waislamu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 13, 2018 21:42 UTC
  • Parnham akiri kuanzisha wimbi la mashambulizi dhidi ya Waislamu Uingereza

Mbaguzi mashuhuri wa rangi wa Uingereza amekiri kwamba amekuwa akiwachochea raia wa nchi hiyo kuwashambulia Waislamu.

Mtandao wa gazeti la Evening Standard umeripori kuwa, mbaguzi mashuhuri wa Uingereza, David Parnham amekiri mahakamani kwamba, alikuwa akiwaandika barua na jumbe nyingi wakazi wa London, Midlands na Yorkshire akiwataka kushambulia misikiti na vituo vya Kiislamu tarehe 3 Aprili mwaka huu wa 2018.

Barua hizo zilitenga alama kwa ajili ya watu watakaowashambulia Waislamu kama vile alama kumi kwa mashambulizi ya maneno, alama 50 kwa kuwamwagia Waislamu tindikali usoni, alama 1,000 kwa mtu atayeshambulia misikiti ya Waislamu kwa bomu na alama 2,500 kwa mtu atakayeshambulia mji mtakatifu wa Makka.

Kwa kipindi cha miaka miwili pia David Parnham alikuwa akituma paketi zenye poda nyeupe kwa wawakishi Waislamu wa Uingereza, wanasiasa mashuhuri na kwenye vituo vya Kiislamu nchini Uingereza ili kuwatia woga na hofu.

Polisi ya Uingereza imesema kwamba, David Parnham ni mwanachama wa kundi la wabaguzi linalojulikana kwa jina la Dylann Roof linalomuenzi mbaguzi mashuhuri wa kizungu aliyekuwa na jina hilo ambaye aliwaua Wamarekani 9 wenye asili ya Afrika katika kanisa moja huko kusini mwa California.