Pompeo akiri kutengwa Washington katika kutekeleza vikwazo dhidi ya Iran
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani amekiri kuwa Washington imetangwa katika kutekeleza vikwazo dhidi ya Iran.
Akizungumza na televisheni ya CBS, Mike Pompeo amekiri kutokuwa na natija hatua za White House dhidi ya Iran na kueleza kuwa nchi za Ulaya hazipasi kuendelea kufanya biashara na Iran. Nchi za Ulaya zimejizuia kuiunga mkono Marekani katika kuiwekea Iran vikwazo bali zimetaka kulindwa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA; hatua inayoweza kuipelekea Marekani kutengwa zaidi kimataifa na nchi waitifaki wake kujiweka kando na Washington.
Wakati huo huo Mawaziri wa Mambo ya Nje na Fedha wa Ujerumani, Uingereza na Ufaransa pamoja na Mkuu wa Siasa za Nje wa Umoja wa Ulaya wametoa taarifa ya pamoja ikibainisha kupiga hatua kubwa mfumo maalumu wa miamala ya kifedha wa umoja huo kwa ajili ya kulinda uhusiano wake wa kibiashara na kibenki na Iran katika kipindi hiki cha vikwazo vya Marekani.