Hillary Clinton: Uchaguzi wa Marekani unatawaliwa na mfumo dume
https://parstoday.ir/sw/news/world-i50260-hillary_clinton_uchaguzi_wa_marekani_unatawaliwa_na_mfumo_dume
Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton ameushambulia mfumo wa uchaguzi wa nchi hiyo akiutaja kuwa unatawaliwa na mfumo dume.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Dec 19, 2018 02:49 UTC
  • Hillary Clinton: Uchaguzi wa Marekani unatawaliwa na mfumo dume

Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton ameushambulia mfumo wa uchaguzi wa nchi hiyo akiutaja kuwa unatawaliwa na mfumo dume.

Clinton ambaye aligombea urais wa Marekani katika uchaguzi uliopita wa mwaka 2016 amesema kuwa, si kazi rahisi kwa mwanamke kugombea katika uchaguzi wa rais wa Marekani. 

Hillary Clinton pia ameshambulia mfumo dume wa uchaguzi wa rais wa Marekani katika barua aliyomwandikia msichana mdogo mwenye umri wa miaka 8 ambaye ameshindwa na mwenzake mwanaume kwa tofauti ya kura moja tu katika uchaguzi wa shule.

Licha ya madai na nara tupu zinazotolewa kuhusu usawa wa kijinsia nchini Marekani, Hillary Clinton alikuwa mwanamke wa kwanza katika historia ya nchi hiyo kuwahi kugombea kiti cha rais mwaka 2016. 

Clinton alipata kura nyingi za wananchi lakini akashindwa na Donald Trump katika idadi ya kura za wajumbe wa majimbo. Trump alipata kura za wajumbe wa majimbo zaidi ya 270 yanayohitajika kumwezesha mgombea kushinda uchaguzi huo.