Dec 26, 2018 02:40 UTC
  • Vyuo Vikuu vya Ujerumani kuanza kutumia mafunzo ya Qurani

Akademia ya Uislamu katika Sayansi na Jamii ya Chuo Kikuu cha Goethe nchini Ujerumani imeunda makundi mawili ya utafiti kwa lengo la kubuni mfumo wa kidijitali wa kuhifadhi maelezo na uchambuzi wa Qurani Tukufu na 'Sheria za Qurani'.

Kwa mujibu wa ripoti ya Chuo Kikuu cha Goethe, akademia hiyo inapania kutumia bajeti ya Yuro milioni 2.7 katika kufanikisha mpango huo.

Chuo Kikuu hicho kimesema mradi huo wa kijamii umeainishwa na kuidhinishwa na Wizara ya Elimu na Utafiti ya Ujerumani, kwa kushirikiana na Wakfu wa Mercator. 

Mbali na Chuo Kikuu cha Goethe, Vyuo Vikuu vyengine vya Ujerumani vinavyoshirikishwa kwenye mradi huo ni pamoja na Frankfurt am Main, Gisen na Hamburg.

 

Maktaba ya Qurani

Tafiti nyingi zimefanywa kuhusu Qurani Tukufu na aghalabu zimehifadhiwa kwa njia ya maandishi, lakini mradi huu wa Akademia ya Uislamu katika Sayansi na Jamii ya Chuo Kikuu cha Goethe nchini Ujerumani unapania kuhifadhi tafiti hizo kupitia mfumo wa dijitali.

Kwa utaratibu huu, taarifa zozote mpya kuhusu historia na chimbuko la Uislamu na pia maelezo kuhusu Qurani Tukufu zitawekwa mtandaoni kwa ajili ya kuwanufaisha watu wote.

 

 

Tags