Uchunguzi: Wamarekani wengi hawaamini vyombo vya habari vya nchi hiyo
https://parstoday.ir/sw/news/world-i5293-uchunguzi_wamarekani_wengi_hawaamini_vyombo_vya_habari_vya_nchi_hiyo
Uchunguzi wa maoni uliofanywa nchini Marekani umeonesha kuwa, idadi kubwa ya Wamarekani hawana imani na vyombo vya habari vya nchi hiyo kutokana na kutokuwa na mitizamo sahihi, upendeleo na kutokuwa na uadilifu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 18, 2016 00:02 UTC
  • Uchunguzi: Wamarekani wengi hawaamini vyombo vya habari vya nchi hiyo

Uchunguzi wa maoni uliofanywa nchini Marekani umeonesha kuwa, idadi kubwa ya Wamarekani hawana imani na vyombo vya habari vya nchi hiyo kutokana na kutokuwa na mitizamo sahihi, upendeleo na kutokuwa na uadilifu.

Uchunguzi wa maoni uliofanywa na The Associated Press-NORC unasema kuwa ni asilimia 6 tu ya Wamarekani ambao wana imani na vyombo vya habari vya nchi hiyo. Uchunguzi huo umebaini kuwa, Wamarekani wengi hufuatilia habari kupitia mitandao ya kijamii kama Facebook na Twitter kwa sababu ya kutokuwa na imani na vyombo vya habari vya nchi hiyo. Uchunguzi wa Associated Press-NORC pia umeenda mbali na kusisitiza kuwa, hata baina Wamarekani wanaofuatilia habari kupitia mitandao hiyo ya kijamii, ni asilimia 12 tu ndio wanaoamini habari wanazosoma au kutazama katika mitandao hiyo.

Vyombo vya habari vya Marekani vimekumbwa na mikasa na kashfa nyingi za kutoa habari zisizo sahihi za ndani na za kimataifa.