ECFR yaitaka Marekani iangalie upya sera zake haribifu dhidi ya JCPOA
https://parstoday.ir/sw/news/world-i53429-ecfr_yaitaka_marekani_iangalie_upya_sera_zake_haribifu_dhidi_ya_jcpoa
Baraza la Uhusiano wa Kigeni la Ulaya ECFR limeitaka Marekani iangalie upya sera zake haribifu na za kiuhasama dhidi ya makubaliano ya nyuklia ya Iran yanayojulikana kama JCPOA.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 12, 2019 02:29 UTC
  • ECFR yaitaka Marekani iangalie upya sera zake haribifu dhidi ya JCPOA

Baraza la Uhusiano wa Kigeni la Ulaya ECFR limeitaka Marekani iangalie upya sera zake haribifu na za kiuhasama dhidi ya makubaliano ya nyuklia ya Iran yanayojulikana kama JCPOA.

Katika barua yake kwa Rais Donald Trump wa Marekani, baraza hilo sambamba na kuashiria kuhusu matokeo hasi ya uamuzi wa Washington wa kujiondoa kwenye mapatano hayo ya kimataifa, limemuasa Trump kutazama upya hatua ya kuiondoa US kwenye JCPOA.

Barua hiyo ya Baraza la Uhusiano wa Kigeni la Ulaya kwa Trump imemtaka rais huyo wa Marekani kuachana na sera za kiuadui dhidi ya taifa la Iran, na kubainisha kwamba kujiondoa Marekani kwenye JCPOA kulidhalilisha thamani na jitihada za pande kadhaa za kidiplomasia.

Jumatano iliyopita, Iran ilitangaza kusimamisha baadhi ya ahadi zake ilizozitoa katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA na kuzipa pande zilizobakia kwenye mapatano hayo muda wa siku 60 kuhakikisha kuwa zinatekeleza ipasavyo ahadi zao.

Nchi zilizosalia kwenye JCPOA baada ya US kujiondoa

Baada ya Rais Hassan Rouhani kutoa tangazo hilo, Umoja wa Ulaya ulitoa taarifa na kutangaza kuwa ungali unaunga mkono JCPOA lakini ukapinga hatua ya Iran kuainisha muhula maalumu wa kuutaka umoja huo utekeleze ahadi zake.

Tarehe 8 mwezi Mei mwaka jana, Trump alitangaza habari ya kuindoa Marekani kwenye makubaliano hayo ya kimataifa sambamba na kuanzisha duru mpya ya vikwazo vya upande mmoja dhidi ya taifa hili.