Heiko Maas asisitiza udharura wa kufanya mazungumzo na Iran
https://parstoday.ir/sw/news/world-i55019-heiko_maas_asisitiza_udharura_wa_kufanya_mazungumzo_na_iran
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani amesisitiza kuwa kuna udharura wa kufanya mazungumzo na Iran. Maas ameyasema hayo katika mazungumzo kwa njia ya simu na Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani Mike Pompeo.
(last modified 2026-02-25T03:34:48+00:00 )
Jul 27, 2019 02:32 UTC
  • Heiko Maas asisitiza udharura wa kufanya mazungumzo na Iran

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani amesisitiza kuwa kuna udharura wa kufanya mazungumzo na Iran. Maas ameyasema hayo katika mazungumzo kwa njia ya simu na Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani Mike Pompeo.

Maas jana alifanya mazungumzo kwa njia ya simu na Mike Pompeo na kusisitiza kuwa hivi sasa tunahitaji udiplomasia na Iran. Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani pia amebainisha kuwa Ujerumani haitaunga mkono siasa za serikali ya Marekani zinazojulikana kama siasa za mashinikizo ya ziada dhidi ya Iran. 

Kuhusu kujiunga Ujerumani na muungano wa Ulaya unaoongozwa na Uingereza kuhusu safari za meli katika eneo la Lango Bahari la Hormoz, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani ameeleza kuwa nchi yake itachukua uamuzi unaopasa baada ya kubainika wazi malengo ya mpango huo na dhumuni la ushiriki wa nchi yake.  

Uingereza ina mkakati wa kuanzisha muungano wa meli za Ulaya katika eneo la Ghuba ya Uajemi hata hivyo nchi hiyo haina meli za kutosha kwa ajili ya kutekeleza mpango wake huo kwa sababu meli na manowari nyingi za nchi hiyo hivi sasa zinafanyiwa ukarabati. Rais Hassan Rouhani iwa Iran amesisitiza kuwa Iran ina jukumu kuu la kulinda na kudhamini usalama wa eneo la Lango Bahari la Hormoz,  Ghuba ya Uajemi na nchi jirani na kuongeza kuwa Iran haitaruhusu nchi yoyote kusababisha ukosefu wa usalama katika Ghuba ya Uajemi na Lango Bahari la Hormoz. Amesema  inachukua hatua kulingana na ukengeukaji unaofanywa na upande wa pili. 

Rais Hassan Rouhani wa Iran