Aug 16, 2019 02:29 UTC
  • Sergei Lavrov: Wamagharibi wameshindwa kutatua matatizo yao

Sergei Lavrov, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Russia amesema kuwa, kiigizo cha Wamagharibi kilichosimama juu ya misingi ya uliberali kimethibitisha kushindwa kwao kutatua matatizo yao.

Sergei Lavrov alisema hayo jana Alkhamisi katika Kongamano la Malezi Kwa Vijana wa Russia huko Moscow ambapo aliashiria mgogoro wa wahajiri huko Ulaya na kusema kuwa, Ulaya baada ya kuiangamiza Libya hivi sasa inataabika na wimbi la wahajiri huku nchi za bara hilo zikitafuta njia ya kulipatia ufumbuzi tatizo hilo.

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Russia ameyyataka madola ya Magharibi kuyapatia ufumbuzi matatizo yao badala ya kujihusisha na masuala ya nchi nyingine

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Russia amekosoa vikali hatua ya Ukraine ya kupuuza utekelezaji wa maklubaliano ya Minsk na kusema kuwa, serikali ya Kiev (Kyiv) haina nia ya kutekeleza makubaliano hayo.

Bendera za Russia na Ukraine

Aidha Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Russia ameyataka madola yanayoiunga mkono serikali ya Ukraine kuishinikiza nchi hiyo ili itekeleze majukumu yake badala ya kuendelea kuiandamana serikali ya Russia kwa tuhuma hizi na zile.

Tangu mwaka 2014 wakati hatamu za uongozi wa nchi ya Ukraine ziliposhikwa na serikali yenye mielekeo ya Kimagharibi na kuunganishwa eneo la Cremia na ardhi ya Russia, uhusiano wa Moscow na Kiev uliporomoka sana na kutawaliwa na mivutano mingi.

Tags