Mar 17, 2020 08:02 UTC
  • Zarif aitaka EU ipuuze vikwazo haramu vya Marekani dhidi ya Iran

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameutaka Umoja wa Ulaya uache kuifuata kibubusa Marekani katika kuliwekea taifa hili vikwazo vya upande mmoja, haramu na visivyo vya kisheria.

Mohammad Javad Zarif ametoa mwito huo katika mazungumzo yake ya simu jana Jumatatu na mwenzake wa Uingereza, Dominic Raab ambapo amesisitiza kuwa, ugaidi wa kiuchumi wa Washington dhidi ya Iran, umekuwa na taathira hasi hususan katika kukabiliana na ugonjwa wa Corona hapa nchini.

Ameitaka serikali ya London ipuuze vikwazo hivyo haramu na vya kikatili vya Marekani dhidi ya taifa hili, kwa kuzingatia misingi ya ubinadamu, na pia kama njia ya kuonyesha mfungamano wa Uingereza kwa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.

Kadhalika kwenye mazungumzo hayo ya simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, Dakta Zarif amezishukuru nchi tatu za EU ambazo ni wananchama wa JCPOA (Ujerumani, Uingereza na Ufaransa) kwa kuipa Iran msaada wa kupambana na Corona.

Madaktari wa Iran kazini masaa 24 kukabiliana na Corona

Mazungumzo hayo ya simu yamekuja saa chache baada ya serikali ya London kukubali kuilipa Iran deni lake la pauni milioni 400.

Siku chache zilizopita, Dakta Zarif aliwaandikia barua mawaziri wenzake wa mambo ya nje wa nchi mbali mbali duniani, akiwaomba wazuie na kukomesha ugaidi wa kiuchumi wa Marekani dhidi ya taifa hili.

Tags