NRC yataka kuondolewa vikwazo Iran, Syria na Venezuela
(last modified Wed, 29 Apr 2020 11:10:06 GMT )
Apr 29, 2020 11:10 UTC
  • NRC yataka kuondolewa vikwazo Iran, Syria na Venezuela

Baraza la Wakimbizi la Norway (NRC) limetoa mwito wa kuondolewa vikwazo nchi kadhaa zikiwemo Jamhuri ya Kiislamu a Iran, Syria na Venezuela wakati huu wa mapambano dhidi ya janga la kimataifa la Corona.

Jan Egeland, Mkuu wa shirika hilo la Norwegian Refugee Council ambaye amewahi kuwa mkuu wa ofisi ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa amesema, licha ya kulegezwa vikwazo vya dawa na chakula, lakini kwa ujumla mashirika ya misaada ya kibinadamu yanakabiliwa na vizingiti vya kuwafikishia misaada ya ya dharura masikini na watu wenye mahitaji wakati huu wa mlipuko wa ugonjwa wa Covid-19 (Corona).

Amesema, "kile tunachotaka kwa hakika ni kuondolewa vikwazo vya kiuchumi dhidi ya mataifa kama Iran, Venezuela na Syria, vikwazo ambavyo vimefanya kazi yetu ya kuwahudumia wenye mahitaji kuwa ngumu."

Shirika hilo la kibinadamu limesema vikwazo hivyo vya Marekani na mataifa mengine makubwa ya Magharibi mbali na kurejesha nyuma jitihada za pamoja za dunia za kukabiliana na virusi hivyo angamizi, lakini pia vimeshadidisha baa la njaa na kuwasababishia matatizo masikini.

Maandamano kupinga vikwazo dhidi ya Iran wakati huu wa Corona

Taasisi nyingi za kimatiafa likiwemo shirika la haki za binadamu la Human Rights Watch zimesisitiza kwamba, vikwazo vya upande mmoja vya Marekani dhidi ya Iran vinapaswa kupunguzwa katika kipindi hiki cha mlipuko wa virusi vya Corona ili nchi hii iweze kudhamini mahitaji yake ya dharura.

Hatua ya Marekani ya kuziwekea vikwazo baadhi ya nchi ikiwemo Iran, imeifanya Tehran ishindwe kudhamini sehemu ya mahitaji yake muhimu kwa ajili ya kukabiliana na virusi hivyo.

Tags