Livingstone: Kubuniwa Israel ni janga kubwa duniani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i6580-livingstone_kubuniwa_israel_ni_janga_kubwa_duniani
Meya wa zamani wa London nchini Uingereza amesema kuanzishwa utawala haramu wa Israel ni janga kubwa la kihistroria ambalo taathira zake hasi zinaendelea kushuhudiwa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 07, 2016 03:41 UTC
  • Livingstone: Kubuniwa Israel ni janga kubwa duniani

Meya wa zamani wa London nchini Uingereza amesema kuanzishwa utawala haramu wa Israel ni janga kubwa la kihistroria ambalo taathira zake hasi zinaendelea kushuhudiwa.

Ken Livingstone amesema kuanzishwa kwa utawala huo wa Kizayuni ni kosa kubwa ambalo limeifanya dunia kuwa katika hatari ya kushuhudia vita vya kinyuklia.

Meya huyo ameiamba kanali ya televisheni ya Kiarabu ya al-Ghad al-Arabi kuwa: "Kuanzishwa kwa utawala haramu wa Israel ni kosa kubwa sana la kihistoria haswa ikizingatiwa kuwa jamii ya Wapalestina imekuwepo kwa zaidi ya miaka 2000."

Ken Livingstone amesema baadhi ya migogoro katika eneo la Mashariki ya Kati isingeshuhudiwa iwapo Wazayuni wangehamishiwa Uingereza na Marekani baada ya Vita vya Pili vya Dunia.

Hivi karibuni, Meya huyo wa zamani wa jijini London aitimuliwa kwenye chama chake cha Leba kwa tuhuma za kutoa matamshi ya kibaguzi dhidi ya Wazayuni.

Aidha aliwahi kugonga vichwa vya habari huko nyuma baada ya kudai kuwa, Adolf Hitler, kiongozi wa zamani wa kinazi wa Ujerumani alikuwa Mzayuni kabla hajakuwa 'wazimu'.