Feb 06, 2021 13:23 UTC
  • Nancy Pelosi
    Nancy Pelosi

Spika wa Kongresi ya Marekani amesema kuwa waungaji mkono wa rais wa zamani wa nchi hiyo, Donald Trump ambao mwezi Januari mwaka huu walishambulia jengo la Kongresi ni magaidi wa ndani ya nchi.

Nancy Pelosi amesema kuwa, watu ambao tarehe sita mwezi uliopita wa Januari walishambulia Kongresi, vilevile walishambulia thamani za Marekani. 

Mwezi uliopita waasi wafuasi wa Donald Trump walishambulia majengo ya Bunge la Marekani na kutishia maisha ya wabunge, wanachama wa chama cha Democratic, wafanyakazi na maafisa wa Kongresi. 

Spika wa Bunge la Marekani, Nancy Pelosi ameyataja mashambulizi hayo kuwa ni jeraha katika kiwiliwili cha demokrasia ya Marekani na kusema kuwa: "Kitendo hicho kilichofanywa na magaidi wa ndani ya nchi hakitasahauliwa na tunatoa wito wa kutendeka haki katika kadhia hii." 

Wafuasi wa Trump wakivamia Kongresi ya Marekani

Wakati wa hujuma hiyo ya wafuasi wa Trump, Kongresi ya Marekani ilikuwa ikihesabu kura za majimbo ya nchi hiyo na kupasisha ushindi wa Joe Biden katika uchaguzi wa rais. Hata hivyo Donald Trump ambaye hakuwa tayari kukubali kushindwa, aliwachochea wafuasi wake kushambulia Bunge la Marekani. Watu wasiopungua sita waliuawa katika hujuma hiyo na wengine kadhaa walijeruhiwa. 

Tags