Vijana wengi Wakristo Marekani wachukizwa na jinai za utawala wa Kizayuni
https://parstoday.ir/sw/news/world-i70562-vijana_wengi_wakristo_marekani_wachukizwa_na_jinai_za_utawala_wa_kizayuni
Uchunguzi mpya wa maoni unaonesha kuwa, uungaji mkono wa vijana wengi Wakristo nchini Marekani umepungua kwa utawala wa Kizayuni wa Israel kutokana na jinai zake dhidi ya watoto na watu wasio na hatia huko Palestina.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 26, 2021 02:40 UTC
  • Vijana wengi Wakristo Marekani wachukizwa na jinai za utawala wa Kizayuni

Uchunguzi mpya wa maoni unaonesha kuwa, uungaji mkono wa vijana wengi Wakristo nchini Marekani umepungua kwa utawala wa Kizayuni wa Israel kutokana na jinai zake dhidi ya watoto na watu wasio na hatia huko Palestina.

Gazeti la Kizayuni la Times of Israel limenukuu matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanywa na watafiti wa chuo kikuu cha mji wa Pembroke huko Carolina Kaskazini nchini Marekani yakionesha kuwa, uungaji mkono wa vijana wa Kikristo nchini humo umepungua sana kwa utawala wa Kizayuni na hivi sasa kuna tofauti kubwa ya mitazamo baina ya vijana Wakristo na wazee wao kuhusu Israel hasa baada ya utawala wa Kizayuni kufanya mashambulio ya kinyama na kiwendawazimu dhidi ya Wapalestina wa Ghaza hivi karibuni.

Matokeo ya uchunguzi huo wa maoni yanaonesha kuwa vijana wengi Wakristo nchini Marekani wamekasirishwa sana na jinai zilizofanywa hivi karibuni na utawala wa Kizayuni na hawaridhishwi na nchi yao kuendelea kuwa muitifaki mkubwa wa Israel.

Jinai za kutisha na za kipunguwani za Israel dhidi ya watoto na wanawake wa Palestina, zimemuumiza kila mwenye hisia za utu duniani

 

Uchunguzi huo wa maoni aidha umeonesha kuwa, kuna uwezekano mkubwa wa kupungua mno uungaji mkono wa Israel nchini Marekani kadiri utawala huo unavyozidi kuonesha unyama na ukatili wake.

Uchunguzi huo wa maoni umefanywa kati ya zaidi ya Wakristo 700 wa Marekani wenye umri wa baina ya miaka 18 na 29. Zoezi hilo limefanyika baina ya mwezi Machi na Aprili mwaka huu wa 2021.

Jinai za kutisha na za kinyama za utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina hasa wanawake na watoto wadogo, zimeziumiza nyoyo za watu wote wenye hisia za binadamu duniani.