Ushirikiano na misimamo ya pamoja ya China na Russia kuhusu Ukraine
https://parstoday.ir/sw/news/world-i80028-ushirikiano_na_misimamo_ya_pamoja_ya_china_na_russia_kuhusu_ukraine
Wang Yi Waziri wa Mambo ya Nje wa China na mwenzake wa Russia Sergei Lavrov wameratibu misimamo ya nchi mbili huko Beijing kuhusu kadhia kama za Ukraine, Afghanistan na hali ya mambo katika Peninsula ya Korea.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 06, 2022 01:11 UTC
  • Ushirikiano na misimamo ya pamoja ya China na Russia kuhusu Ukraine

Wang Yi Waziri wa Mambo ya Nje wa China na mwenzake wa Russia Sergei Lavrov wameratibu misimamo ya nchi mbili huko Beijing kuhusu kadhia kama za Ukraine, Afghanistan na hali ya mambo katika Peninsula ya Korea.

Pamoja na hayo, kuna umuhimu kwa Russia kuhusu China kuunga mkono misimamo ya Moscow mkabala wa kadhia ya Ukraine. Hii ni kwa sababu Marekani na pande nyingine za Magharibi zinajaribu kila ziwezalo kuipa Ukraine uanachama ndani ya Nato na hivyo si tu kuufanya muungano huo kuwa jirani na Russia bali pia ili kuidhibiti pakubwa kijeshi nchi hiyo. Ndio maana Moscow mara kadhaa imezitahadharisha Marekani na nchi nyingine za Magharibi kuhusu taathira za vitisho kwa usalama wake. Wakati huo huo, Russia inahiitajia pia China iunge mkono misimamo yake kuhusu Ukraine kwa kuzingatia kunufaika muungano wa Marekani na Ulaya na nguvu ya kijeshi ya Nato mkabala wa Russia. Hii ni kwa sababu chokochoko na vita vya kisaikolojia vinavyoibuliwa na Magharibi kwamba kuna uwezekano Russia kutekeleza mashambulizi dhidi ya Ukraine yanaimarisha nafasi ya kijeshi ya nchi hizo kandokando ya Russia. Kwa msingi huo duru za Magharibi zinaitazama hali hii ya mambo kuwa fursa nzuri ya kutahini uhusiano wa kistratejia kati ya Beijing na Moscow mkabala wa nchi za Magharibi.  

Mvutano baina ya Russia na Ukraine 

Stephen Giddy mchambuzi wa masuala ya kimataifa anasema kuhusiana na suala hilo kuwa: "Hata kama China kihistoria imejizuia kujiingiza katika muungano wowote rasmi lakini haiwezekani kupuuza uhusiano wa kijeshi kati ya China na Russia kwa maslahi ya kitaifa ya nchi mbili hizo. Wakati huo huo hatua za China mkabala wa kuwepo kijeshi nchi za Magharibi khususan Marekani katika maeneo ya maslahi ya pamoja ya Beijing na Moscow zinaweza kuitumbukiza Washington na waitifaki wake mashakani. Hatua za kihafidhina za China kivitendo zimedhihirisha kuwa haina nia ya kukwaruzana na kukabiliana kijeshi na Magharibi ili kuwa dola kuu duniani. Hata hivyo mtazamo huu hauwezi haujumuishi maslahi na mitazamo yote ya Moscow na Beijing.  

Ala Kulli hal, hata kama duru za Magharibi zinasema kuwa hazina matarajio makubwa kuhusu uungaji mkono wa kweli wa China kwa Russia katika hali ya dharura; lakini  inaonekana kuwa nchi mbili hizo zinawiana na kwenda sambamba kimataifa huku zikiwa zimezingirwa na Marekani hadi katika ukanda wa maji ya kandokando ya China; ambapo sasa Beijing na Moscow zinahisi udharura mkubwa wa kuchukua msimamo wa pamoja mbele ya vitisho hivyo vya Magharibi; msimamo wa pamoja ambao utapelekea Marekani kwa kiasi fulani itekeleze siasa zake kwa tahadhari mkabala wa Beijing na Moscow. 

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa China na Russia na jumbe zao mjini Beijing Februari 3, 2022