Wajerumani, Wacyprus na Wagiriki waandamana kuinga mkono Russia
Wananchi wa Ujerumani, Cyprus na Ugiriki wamefanya maandamano wakiiunga mkono Russia na kupinga hatua zilizochukuliwa na madola ya Magharibi na vikwazo vyao dhidi ya nchi hiyo.
Kufuatia kuondolewa kwa wanajeshi wa Russia katika viunga vya Kiev, vyombo vya habari vya Magharibi siku ya Jumapili vilichapisha picha za mji wa Bucha karibu na Kiev vikidai kuwa vikosi vya Russia viliwafyatulia risasi raia walipokuwa wakiondoka katika mji mkuu wa Ukraine.
Ukraine inaituhumu Russia kuwa imehusika na tukio hilo lakini Moscow imekana vikali madai hayo ikisema ni uongo mtupu.
Kwa mujibu wa shirika la Sputnik; Wizara ya Ulinzi ya Rusia imesema katika taarifa kwamba: "Vitengo vyote vya jeshi la Russia viliondoka kabisa Bucha mnamo Machi 30, siku moja baada ya mazungumzo ya ana kwa ana kati ya Russia na Ukraine nchini Uturuki."
Mamia ya wananchi wa Ugiriki waliokiwa na bendera za nchi yao na Russia, wamefanya maandamano ya magari na mapikipiki katika mitaa ya mji mkuu wa nchi hiyo, Athens wakitangaza mshikamano wao wa Russia.
Maandamano mengine kama hayo yamefanyika mjini Berlin huko Ujerumani ambako raia hao waliokuwa na bendera za Russia, walipiga nara za kupinga ushiriki wa nchi yao katika kampeni ya vikwazo dhidi ya Russia na ubaguzi unaofanywa dhidi ya watu wanaozungumza Kirusi.
Maandamana ya wananchi ya kuiunga mkono Russia mjini Berlin yameishia kwenye mnara wa kumbukumbu ya mwanajeshi wa Urusi ya zamani ambao ni nembo ya ukombozi wa Ujerumani kutoka kwenye makucha ya Manazi.
Huko Syprus pia waandamanaji waliokuwa na bendera za Russia wametangaza uungaji mkono wao kwa nchi hiyo wakitaja kuwa ni mdhamini wa usalama wa wa kimataifa.
Russia imekuwa chini ya mashinikizo makubwa ya kiuchumi, kijeshi na kiusalama ya nchi za Magharibi hasa Marekani baada ya kuishambulia Ukraine Februari 24 mwaka huu.