Mbunge wa Uingereza afariki dunia baada ya kujeruhiwa kwa risasi
https://parstoday.ir/sw/news/world-i9328-mbunge_wa_uingereza_afariki_dunia_baada_ya_kujeruhiwa_kwa_risasi
Mbunge wa Uingereza Jo Cox amefariki dunia kutokana na majeraha aliyopata baada ya kupigwa risasi jana.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jun 17, 2016 04:27 UTC
  • Mbunge wa Uingereza afariki dunia baada ya kujeruhiwa kwa risasi

Mbunge wa Uingereza Jo Cox amefariki dunia kutokana na majeraha aliyopata baada ya kupigwa risasi jana.

Vyombo vya habari vya Uingereza vimeripoti kuwa Jo Cox aliyekuwa mbunge wa chama cha Labour, amefariki dunia kutokana na majeraha makali.

Polisi ya Uingereza imemtia nguvuni bwana mmoja mwenye umri wa miaka 52 kwa tuhuma za kumpiga risasi mbunge huyo.

Jo Cox alipigwa risasi na kudungwa kisu jana alipokuwa akizungumza na wananchi katika eneo la Birstall huko kaskazini mwa Uingereza.

Bi Cox alikuwa miongoni mwa wabunge wanaounga mkono suala la Uingereza kubakia katika Umoja wa Ulaya na ameuawa wiki moja tu kabla ya kura muhimu ya maoni ya kuamua iwapo nchi hiyo utabakia katika umoja huo au la. Vilevile Cox alikuwa muungaji mkono mkubwa wa suala la kukaribishwa wakimbizi hususan watoto kutoka Syria nchini Uingereza.