Netanyahu afanikiwa kuwatoroka waandamanaji kwa msaada wa polisi ya Uingereza
Mar 26, 2023 07:35 UTC
Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel amefanikiwa kuwatoroka waandamanaji mjini London, Uingereza kwa msaada wa polisi ya mji huo.
Maandamano dhidi ya utawala wa Kizayuni nchini Uingereza yameongezeka katika miezi ya hivi karibuni kutokana na kushadidi jinai na mashambulizi ya kinyama ya utawala wa Kizayuni dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina.
Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, baada ya waziri mkuu wa utawala haramu wa Israel Benjamin Netanyahu kuondoka London, polisi wa Uingereza walilazimika kuweka kizuizi cha barabarani kuwazuia waandamanaji ili kiongozi huyo wa wazayuni aweze kufika uwanja wa ndege.
Hayo yamejiri huku zaidi ya Wazayuni 200,000 wakifanya maandamano makubwa mjini Tel Aviv pekee dhidi ya mpango tata wa Netanyahu wa kurekebisha mfumo wa mahakama wa utawala wa Kizayuni.
Maandamano hayo ya Tel Aviv yalikuwa makubwa kiasi kwamba polisi wa utawala wa Kizayuni walilazimika kutumia nguvu na mabavu, ambapo kufuatia hatua hiyo ya vikosi vya usalama vya Kizayuni, maandamano hayo yaligeuka kuwa ya vurugu na kupelekea watu kadhaa kujeruhiwa.
Maandamano katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu ya Palestina yanaendelea kwa wiki ya kumi na mbili mfululizo kupinga mpango tata wa Netanyahu na baraza lake la mawaziri.
Siku ya Alhamisi usiku, Netanyahu alikataa kusimamishwa kwa namna yoyote ile mpango wa mageuzi ya mfumo wa mahakama wa Israel.
Katika upande mwingine, mamia ya waandamanaji wanaopinga ziara ya hivi karibuni ya waziri mkuu huyo wa utawala wa Kizayuni nchini Uingereza walifanya maandamano mbele ya jengo la Waziri Mkuu wa nchi hiyo, wakipiga nara za "Mauti kwa Israel" na kuonesha kuchukizwa kwao na uungaji mkono wa serikali ya Uingereza kwa utawala huo mtenda jinai.
Vyama vya siasa vya upinzani nchini Uingereza pia vimetangaza upinzani wao mkali dhidi ya ziara ya Netanyahu mjini London sambamba na maandamano ya nchini humo na ukosoaji wa kimataifa dhidi ya utawala wa Kizayuni na kuitaka Uingereza ijitenge na utawala dhalimu wa Kizayuni wa Israel.../
Tags