Russia yaamuru kukamatwa Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu
https://parstoday.ir/sw/news/world-i97572-russia_yaamuru_kukamatwa_mwendesha_mashtaka_wa_mahakama_ya_kimataifa_ya_uhalifu
Kufuatia tuhuma za uwongo zilizotolewa na Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) dhidi ya Rais wa Russia, nchi hiyo imetoa amri ya kukamatwa mwendesha mashtaka huyo.
(last modified 2025-10-23T11:19:28+00:00 )
May 20, 2023 06:20 UTC
  • Karim Khan
    Karim Khan

Kufuatia tuhuma za uwongo zilizotolewa na Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) dhidi ya Rais wa Russia, nchi hiyo imetoa amri ya kukamatwa mwendesha mashtaka huyo.

Serikali ya Moscow ililipiza kisasi cha hatua ya mahakama ya ICC kwa kumuweka Mwendesha Mashtaka Mkuu wa mahakama hiyo, Karim Khan kwenye orodha ya watu wanaosakwa baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu mjini The Hague kutoa hati ya kukamatwa Rais wa Russia, Vladimir Putin, kufuatia tuhuma za uongo zilizotolewa Karim Khan, dhidi ya Putin kuhusiana na watoto waliodaiwa kutekwa nyara huko Ukraine.

Mwezi Machi 2023, Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ilitoa hati ya kukamatwa Rais Putin na Kamishna wa Haki za Watoto wa Russia, Maria Lova Belova, kwa tuhuma za uongo eti kuhusika na uhalifu wa kivita nchini Ukraine na kuwahamisha kinyume cha sheria watoto na raia wengine wa Ukraine hadi Russia 

Kutolewa kwa hati ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ya kukamatwa Putin kumeibua hisia kali kutoka Kremlin na kwa washirika wa Rais wa Russia.

Akitoa jibu kwa hati hiyo ya kukamatwa Rais Putin, Dmitry Medvedev, Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Taifa la Russia, alitoa wito wa kufanyika shambulizi la kombora dhidi ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu huko Uholanzi.

Vyacheslav Volodin, Spika wa Bunge la Russia, Duma, pia alisema kuwa hati hiyo ni sawa na kitendo cha uvamizi dhidi ya nchi hiyo.