Iran yaitaka serikali ya Ufaransa iache kuwakandamiza waandamanaji
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema Polisi ya Ufaransa inapaswa kujizuia kutumia mabavu dhidi ya waandamanaji wanalalamikia kuuawa kijana wa miaka 17 mikononi mwa polisi
Kwa mujibu wa Shirika Rasmi la Habari la Iran, IRNA, Nasser Kanaani Chafi, Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran ameongeza kuwa wakuu wa Ufaransa wanapaswa kusikiliza matakwa ya waandamanaji.
Aidha amesema: "Miamala ya kibaguzi dhidi yawahajiri na kukataa kurekebisha mienendo isiyo sahihi inayofanywa na baadhi ya nchi za Ulaya kumesababisha hali mbaya kwa raia wa Ulaya wakiwemo wa Ufaransa."
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema: "Inatarajiwa kuwa serikali ya Ufaransa itahitimisha ukatili dhidi ya watu wake kwa kuheshimu misingi ya utu, uhuru wa kusema na haki ya raia kufanya maandamano ya amani."
Huku akisisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inafuatilia kwa karibu matukio ya hivi sasa nchini Ufaransa, Kanaani Chafi alisema: "Kutokana na hali ya ukosefu wa usalama na isiyotabirika ya Ufaransa, tunawaomba raia wa Iran wanaoishi katika nchi hii wajiepusha na shughuli zisizo za dharura katika miji nchin humo na pia wajizuie kuenda katika maeneo yenye mapigano."

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Iran pia amewataka raia wa Iran kuepuka safari zisizo za lazima Ufaransa wakati huu wa mgogoro nchini humo.
Kufuatia ghasia hizo za Ufaransa, Ravina Shamdasani, msemaji wa Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, amesema Umoja wa Mataifa una wasiwasi kuhusu mauaji ya kijana aliyekuwa na umri wa miaka 17 mwenye asili ya Afrika Kaskazini akiwa mikononi mwa polisi nchini Ufaransa siku ya Jumanne iliyopita".
Afrisa huyo wa Umoja wa Mataifa ameongeza kuwa: "Umewadia wakati wa Ufaransa kushughulikia ipasavyo matatizo ya ubaguzi na ubaguzi wa rangi ambayo yamekita mizizi katika katika utekelezaji wa sheria." Taasisi hiyo ya kimataifa pia imetoa wito wa kuamiliana kibinadamu na raia wanaoandamana.