Oct 01, 2023 02:36 UTC
  • Jumapili, Mosi Oktoba, 2023

Leo ni Jumapili tarehe 15 Mfunguo Sita Rabiul-Awwal 1445 Hijria sawa na tarehe Mosi Oktoba 2023 Miladia.

Siku kama ya leo miaka 151 iliyopita, Muhammad Qazvini, mwanafasihi, mhakiki na mwanahistoria alizaliwa katika mji wa Tehran, mji mkuu wa Iran. Alijifunza misingi ya fasihi na elimu ya teolojia akiwa katika rika la ubarobaro. Muhammad Qazvini alionyeshha kipaji cha hali ya juu katika masomo ambapo alijifunza fasihi kwa baba yake na kwa wanafasihi wa zama hizo. Kipindi fulani aliishi Ulaya ambapo akiwa huku alitumia fursa hiyo kuandika kukopi kwa kuandika nakala za vitabu vya lugha ya Kifarsi vilivyokuwa vikipatikana katika makumbusho barani Ulaya. Moja ya athari muhimu za Muhammad Qazvini ni kitabu cha Tarikh va Zendegi dar asr Hafez. Alimu huyu aliaga dunia katika mji wa Rey ulioko kusini mwa Tehran na kuzikwa huko. ***

 

Miaka 74 iliyopita katika siku kama ya leo, kuasisiwa kwa Jamhuri ya Watu wa China kulitangazwa rasmi, na Mao Tse Tung akachaguliwa kuwa rais wa jamhuri hiyo. Nchi ya China yenye ustaarabu mkongwe, ilikuwa chini ya udhibiti wa madola ya Ulaya kuanzia mwishoni mwa karne ya 16. Mara kadhaa Wachina walianzisha vita dhidi ya mkoloni hasa Muingereza ili kuikomboa nchi yao lakini hawakufanikiwa. Mwaka 1912 mapinduzi yaliyoongozwa na Sun Yat-Sen dhidi ya mfumo wa utawala wa Kifalme yalizaa matunda na kiongozi huyo akachaguliwa kuwa rais wa China. ***

Bendera ya China

 

Katika siku kama ya leo miaka 63 iliyopita, nchi ya Nigeria ilipata uhuru. Wareno waliwasili Nigeria katika karne ya 15 na mkoloni Mwingereza naye akawasili katika nchi hiyo katika karne ya 16. Katika karne ya 17 ardhi ya Nigeria iligeuzwa na kuwa moja kati ya vituo muhimu vya biashara ya utumwa. Mwishoni mwa karne ya 19 vikosi vya majeshi ya Uingereza, viliidhibiti kikamilifu ardhi ya Nigeria. Mwaka 1914 Uingereza uliziunganisha nchi mbili za Nigeria ya Kaskazini na Kusini zilizokuwa chini ya udhibiti wake na kuunda koloni moja la Nigeria. Miaka 40 baadaye nchi hiyo ikajitangazia kuwa na utawala wa ndani. Hatimaye baada ya kupitia misukosuko mingi, Nigeria ikajipatia uhuru katika siku kama ya leo. ***

Bendera ya Nigeria

 

Siku kama ya leo mika 33 iliyopita, aliaga dunia Siraj Munir, mhakiki maarufu wa Kipakistani. Siraj Munir mhakiki na mwandishi mkkubwa wa Kipakistan alizaliwa mwaka 1952. Kutokana na mapenzi yake makubwa kwa utamaduni, lugha, na fasihi ya lugha ya Kifarsi, amefanya huduma kubwa ya kueneza lugha hii nchini Pakistan sambamba na kuwatambulisha shakhsia mashuhuri wa Kiirani katika uga wa fasihi, utamaduni na falsafa. ***

 

Katika siku kama ya leo miaka 27 iliyopita, aliaga dunia Ayatullah Sayyid Muhammad Husseini mashuhuri kwa jina la Agha Najafi Hamedani. Alizaliwa Najaf Iraq. Alielekea katika mji wa Hamedan Iran akiwa pamoja na baba yake. Akiwa na umri wa miaka 21 Sayyid Muhammad Husseini alifunga safari na kuelekea katikia Hawaza ya Najaf Iraq kwa ajili ya kujiendeleza zaidi kielimu. Baada ya kuishi kwa miaka 22 huko Najaf alirejea Hamedan akiwa na idhinio ya Ijtihad kutoka kkwa Maulamaa tofauti. ***

 

Na tarehe Mosi Oktoba ni siku ya Wazee Duniani. Siku hii ilitengwa kwa ajili ya kuwakirimu na kuwaenzi watu wa tabaka hilo. Ni vyema kukumbusha hapa kuwa hapa nchini Iran na kutokana na mabadiliko yaliyotokea baada ya Mapinduzi ya Kiislamu na utamaduni wa Kiislamu unaotawala hapa nchini wazee na watu wazima wanapewa nafasi ya juu ndani ya familia na katika jamii. ***

 

Tags