Mar 16, 2018 02:00 UTC
  • Ijumaa tarehe 16 Machi 2018

Leo ni Ijumaa tarehe 27 Jamadithani 1439 Hijria sawa na Machi 16, 2018

Siku kama ya leo miaka 30 iliyopita, utawala wa Baath nchini Iraq uliushambulia bila huruma na kwa mabomu ya kemikali za sumu mji wa Halabcha wa wakazi wa Kikurdi huko kaskazini mashariki mwa nchi hiyo kwa kutumia makumi ya ndege za kivita. Hujuma hiyo ilianza baada ya kushindwa kupambana na wapiganaji Waislamu wa Iran na wa Kikurdi wa huko Iraq, na katika upande wa pili wananchi Waislamu wa Halabcha waliwakaribisha wapiganaji wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kutokana na dhulma na ukandamizaji usio na kipimo wa Saddam Hussein dhidi yao. Raia elfu tano wasio na hatia waliuawa kutokana na kuvuta gesi ya sumu huko Halabcha. Hata hivyo nchi za Magharibi hazikuchukua hatua yoyote mbele ya jinai hiyo kubwa na ya kutisha.

Halabcha

Siku kama ya leo miaka 78 iliyopita, alifariki dunia Bi Selma Lagerlof mwandishi wa Sweden. Lagerlof alizaliwa mwaka 1858 na baada ya kumaliza masomo yake akaanza kujishughulisha na ukufunzi na uandishi wa hadithi na hekaya. Lagerlof alikuwa mwanamke wa kwanza kutunukiwa tuzo ya Nobel katika fani ya fasihi mwaka 1909.

Bi Selma Lagerlof

Katika siku kama ya leo miaka 159 iliyopita Alexander Stepanovich Popov, mvumbuzi na mwanafizikia wa Russia alizaliwa. Baada ya kuhitimu masomo yake katika taaluma ya fizikia, alianza kujishughulisha na ufundishaji katika vyuo vikuu vya nchi hiyo. Mbali na shughuli hiyo, Popov aliendelea mbele na utafiti wake katika nyanja mbalimbali za kielimu ambapo baadaye alifanikiwa kuvumbua chombo cha kunasia sauti na kukipa jina la kinasia sauti. Aliaga dunia mwaka 1906.

Na siku kama ya leo miaka 1048 iliyopita, alifariki dunia mtaalamu wa mashairi wa Kiislamu kwa jina la Ibn Hajjaj. Ibn Hajjaj alizaliwa mjini Baghdad, Iraq na alijikita katika taaluma ya mashairi akkiwa bado kijana na kutokea kuwa maarufu katika uwanja huo. Alitunga mashairi mengi yanayowaenzi na kuwasifu Ahlul bait wa Mtume (saw) na kuwashambulia wapiznani wa Uislamu na Mtume. Miongoni mwa athari za malenga huyo ni pamoja na diwani ya mashairi yenye juzuu kumi inayohifadhiwa katika maktaba mbalimbali duniani.