Apr 12, 2018 22:04 UTC
  • Ijumaa, Aprili 13, 2018

Leo ni Ijumaa tarehe 26 Rajab 1439 Hijria sawa na tarehe 13 Aprili 2018 Milaadia.

Siku kama ya leo miaka 1442 iliyopita kwa mujibu wa baadhi ya mapokezi ya historia, Abu Twalib ami ya Mtume Muhammad (SAW) na baba wa Imam Ali (A.S) alifariki dunia wakati Waislamu walipokuwa chini ya mzingiro wa washirikina wa Makka. Abu Twalib alikuwa pamoja na Waislamu wengine huko katika Shiibi Abi Twalib akimlinda na kumhami mtukufu huyo mbele ya adha za washirikina. Mtume Muhammad (SAW) alikuwa chini ya uangalizi wa Abu Twalib tangu alipokuwa na umri wa miaka minane, baada ya kuaga dunia babu yake Abdul Muttalib. Abu Twalib alisilimu baada ya kubaathiwa Mtume na alikuwa muungaji mkono na mtetezi mkubwa wa Mtume Mtukufu dhidi ya washirikina wa Kikuraishi.

Siku kama ya leo miaka 99 iliyopita, kulijiri tukio la umwagaji damu mkubwa katika Bustani ya Jallianwala Bagh nchini India. Mwaka 1919 na kwa lengo la kuzuia uasi na mapambano ya wananchi, serikali ya kikoloni ya Uingereza ilipasisha sheria iliyowapa polisi haki ya kuwatia mbaroni wanaharakati wa India bila sababu yoyote na kuwashikilia kwa muda usiojulikana. Sheria hiyo iliwakasirisha mno wananchi wa India na katika siku kama ya leo zaidi ya Wahindi elfu tano waliokuwa wamekusanyika kwa amani katika Bustani ya Jallianwala katika mji wa Amritsar walimiminiwa risasi kwa amri ya kamanda mmoja wa Uingereza. Watu 1200 waliuawa na wengine 4000 kujeruhiwa katika tukio hilo. Baada ya mauaji hayo, harakati ya ukombozi wa India ikiongozwa na shujaa Mahatma Ghandhi ilipamba moto.

گاندی، رهبر مبارزه با استعمار انگلستان در هند

Siku kama ya leo miaka 43 iliyopita, shambulio la wanamgambo wa Kikristo wenye misimamo ya kufurutu ada wa kundi la Mafalanja lililolenga basi moja lililokuwa na Wapalestina na kuua watu 30 kati yao, lilipelekea kuibuka vita vya ndani nchini Lebanon. kufuatia mauaji hayo, Waislamu na wazalendo wa Lebanon walianzisha mapambano ya kukabiliana na Mafalanja hao. Muda mfupi baadaye harakati za wapiganaji wa Kipalestina pia ziliingia katika vita hivyo vya ndani vya Lebanon. Vita hivyo ambayo vilikuwa vikichochewa na utawala haramu wa Israel, viliisababishia hasara kubwa ya mali na roho serikali ya Beirut.

wanamgambo wa Kikristo katika viunga vya Beirut

Siku kama ya leo miaka 32 iliyopita, alifariki dunia msomi mkubwa wa Kiislamu, Ayatullah Mujtaba Hatami Lankarani. Ayatullah Lankarani alizaliwa katika mji wa Isfahan hapa nchini Iran na katika kipindi cha ujanani alielekea katika mji wa Najaf huko Iraq kwa ajili ya kupata masomo. Akiwa huko Najaf, Ayatullah Mujtaba Hatami Lankarani aliweza kusoma chini ya maulama wakubwa wa zama zake kama vile Dhiyaudin Iraqi, Ayatullah Mirzai Naayini na Sayyid Abul-Hassan Isfahani. Baada ya kumaliza masomo yake na kufikia daraja ya juu ya elimu alirudi katika mji alikozaliwa wa Isfahan na kutumia umri wake wote katika kutoa mafunzo ya dini tukufu ya Kiislamu. Ayatullah Lankarani alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 75.

Ayatullah Mujtaba Hatami Lankarani