May 13, 2018 03:27 UTC
  • Jumapili, Mei 13, 2018

Leo ni Jumapili tarehe 26 Sha'ban 1439 Hijiria, sawa na tarehe 13 Mei 2018 Miladia.

Siku kama ya leo miaka 1334 iliyopita, alifariki dunia, Yazid bin Abdul-Malik bin Marwan, khalifa dhalimu wa wakati huo. Yazid bin Abdul-Malik aliingia madarakani baada ya kufariki dunia Omar bin Abdul-Aziz hapo mwaka 101 Hijiria. Kiongozi huyo mbali na kufanya dhulma na ukandamizaji, hakuzingatia pia masuala ya Waislamu. Kwa kuzingatia kuwa alikuwa ni mtu wa karibu na ukoo wa Hajjaj Thaqafi, hivyo aliwapa umuhimu mkubwa watu wa ukoo huo.

Yazid bin Abdul-Malik

Siku kama ya leo miaka 684 iliyopita, alifariki dunia Ibn Faswih, aliyekuwa faqihi, malenga na mtaalamu wa lugha ya Kiarabu, huko mjini Damascus, Syria. Baada ya kusoma elimu ya sheria za Kiislamu na lugha ya Kiarabu, alianza kujifundisha pia elimu ya hadithi na kufikia ujuzi wa hali ya juu katika uwanja huo. Aidha msomi huyo mbali na elimu za dini, alisoma pia mashairi huku akiandika vitabu mbalimbali kuhusu maudhui tofauti ikiwemo fiqhi.

Siku kama ya leo miaka 305 iliyopita alizaliwa mjini Paris Alexis Cloude Clairaut mwanahesabati mashuhuri wa Ufaransa. Alikuwa na hamu kubwa na somo la hesabati ambapo akiwa na umri mdogo wa miaka 18 alifanikiwa kujiunga na Chuo cha Sayansi cha Ufaransa. Clairaut alipata umashuhuri mkubwa duniani kutokana na utafiti makini aliofanya katika nyanya tofauti za sayansi. Msomi huyo aliaga dunia mwaka 1765.

Alexis Cloude Clairaut

Siku kama ya leo miaka 265 iliyopita, alizaliwa Lazar Carnot, mwanasiasa, jenerali na mtaalamu wa hisabati wa nchini Ufaransa. Msomi huyo anayehesabika kuwa mmoja wa waasisi wa elimu mpya ya uhandisi, alitabahari pia katika fani ya uhandisi na stratijia ya kijeshi huku akiwa mmoja wa viongozi wenye taathira wa ushindi tofauti wa wanamapinduzi wa nchi hiyo. Ni kwa ajili hiyo ndio maana akaitwa kwa lakabu ya 'roho ya kijeshi ya mapinduzi ya Ufaransa.' Baada ya ushindi wa mapinduzi ya nchi hiyo alishikilia nyadhifa mbalimbali za uongozi ikiwemo nafasi ya uanachama wa mkutano mkuu wa chama tawala na Wizara ya Vita ya Ufaransa. Lazar Carnot alifariki dunia mwaka 1823 Miladia.

Lazar Carnot,

Siku kama ya leo miaka 111 iliyopita, alizaliwa Bi Daphne du Maurier mwandishi wa riwaya, wasifu na thamthiliya wa Kiingereza. Maurier alizaliwa katika familia ya wasanii na iliyokuwa pia na wataalamu wa fasihi. Ni kutokana na kukulia katika mazingira kama hayo, ndipo Bi Daphne du Maurier akafanikiwa kukuza kipaji chake katika uwanja wa uandishi. Miongoni mwa vitabu vyake mashuhuri ni Scapegoat na Rebecca. Mwandishi huyo aliaga dunia mwaka 1889.

Daphne du Maurier

Siku kama ya leo miaka 39 iliyopita kulingana na kalenda ya Hijria Shamsiya, mkataba wa kutoshtakiwa Wamarekani nchini Iran au Capitulation Accord ulifutwa nchini kufuatia mapambano yasiyosita ya wananchi Waislamu wa Iran, ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kuasisiwa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu nchini. Kwa mujibu wa mkataba huo, raia wa Marekani aliyekuwa nchini Iran alikuwa na kinga kamili ya kisheria dhidi ya kufunguliwa mashtaka. Kwa kadiri kwamba hakuna taasisi au chombo chochote cha kisheria cha Iran kilichokuwa na mamlaka ya kumfungulia mashtaka na kumuhukumu raia wa Marekani aliyekuwa akiishi Iran na kesi za raia hao wa Kimarekani zilipaswa kusikilizwa nchini kwao.

Mkataba wa Capitulation Accord

Na siku kama ya leo miaka 18 iliyopita, alifariki dunia Ayatullah Sayyid Mahdi Ruhani, faqihi na msomi mkubwa wa elimu ya theolojia ya Kiislamu. Sayyid Mahdi Ruhani alizaliwa mjini Qum, Iran mwaka 1343 Hijiria. Akiwa kijana Sayyid Mahdi Ruhani alijifundisha elimu ya dini na alipofikisha umri wa miaka 20 akaelekea mjini Najaf, Iraq. Baada ya Ayatullah Sayyid Hossein Borujerdi kuwasili mjini Qum, Ayatullah Mahdi Ruhani alishiriki darsa zake na kusoma kwake elimu ya fiqhi na usulu fiqhi ambapo baada ya muda fulani alianza kufundisha masomo ya ngazi ya juu. Kadhalika Ayatullah Sayyid Mahdi Ruhani alifanya kazi kubwa ya kulinganisha vitabu vya mbinguni kama vile taurati, Injili na Qur'an Tukufu kuhusu nukta shirikishi na zenye kutofautiana. Msomi huyo mtajika alikuwa alimu wa kwanza katika hauza ya kielimu ya mjini Qum kuanza kufundisha elimu za umaksi na dialectic. Aidha aliunga mkono harakati za mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran chini ya uongozi wa Imam Khomeini (MA). Ayatullah Sayyid Mahdi Ruhani alifariki dunia katika siku kama ya leo akiwa na umri wa miakka 76 na kuzikwa karibu na Haram ya Bibi Fatwimat Ma'asuma (as).

Ayatullah Sayyid Mahdi Ruhani