Apr 12, 2019 04:27 UTC
  • Ijumaa, tarehe 12 Aprili, 2019

Leo ni Ijumaa tarehe 6 Sha'aban mwaka 1440 Hijiria, sawa na tarehe 12 Aprili 2019 Miladia.

Siku kama ya leo miaka 1282 iliyopita, Zaid bin Ali bin Hussein, mjukuu wa Imam wa Tatu wa Waislamu wa Kishia, alipeperusha bendera ya harakati yake huko mjini Kufa, Iraq wakati wa utawala wa Bani Umayyah. Mapambano ya Zaid ambayo wafuasi wake walitambuliwa kwa jina la Zaidiyyah, yalidumu kwa muda mrefu ambapo mwaka 739 Miladia, aliuawa na Yusuf Ibn Omar Thaqafi, mmoja wa watawala wa Bani Umayyah. Kufuatia matukio hayo, baadhi ya wafuasi wa kiongozi huyo (Zaid bin Ali) ambao hawakuwa Wairani walihamia nchini Yemen na tangu wakati huo Yemen inajulikana kama kituo kikuu cha Waislamu wa Shia Zaidiyyah. Ni bora ikafahamika kuwa, hii leo nusu ya jamii ya Wayemen inaundwa na Mashia Zaidiyyah, Shia Ithna Ashariyyah na Shia Ismailia. Maeneo ambayo wanapatikana zaidi ni kaskazini mwa nchi hiyo.

Zaid bin Ali bin Hussein

Siku kama ya leo miaka 199 iliyopita dawa ya kutibu ugonjwa wa malaria iligundulika kutoka kwenye magamba ya mti wa Cinchona. Asili ya mti huu wenye majani ya kijani kibichi ni maeneo ya Amerika ya Kusini lakini hii leo unapandwa katika ameneo mengine ya dunia. Utomvu wa mti huu hutumika kutengeneza dawa chungu sana ya Quinine. Tarehe 12 Aprili mwaka 1820 kwa mara ya kwanza kabisa madaktari Pierre Joseph Pelletier na Joseph Bienaimé Caventou wa Ufaransa walifanyika majaribio dawa hiyo ya malaria katika Maabara ya Paris na kukaanza jitihada za kuzalisha dawa ya Quinine. 

Siku kama ya leo miaka 196 iliyopita alizaliwa Alexandr Ostrovsky mwandishi wa maonyesho mwenye juhudi wa nchini Russia. Alihitimu masomo ya sheria katika chuo kikuu ingawa aliamua kujiunga na tasnia ya uandishi wa maonyesho. Karibu kila mwaka Alexandr Ostrovsky alikuwa akifanya maonyesho ya kihistoria au kuandika vichekesho ambapo alikuwa akiakisi hali jamii. Alikuwa na taathira kubwa katika senema ya Russia. Miongoni mwa athari za mwanasanaa huyo ni pamoja na 'Binti wa Barafu' 'Msitu' 'Tufani' na 'Muhanga Mwingine.' Mwandishi huyo alifariki dunia mwaka 1886 Miladia.

Alexandr Ostrovsky

Siku kama ya leo miaka 152 iliyopita Mutsuhito, mfalme maarufu wa na mwana mabadiliko wa Japan aliingia madarakani nchini humo. Mfalme huyo aliingia madarakani wakati ambapo Japan ilikuwa inakabiliwa na changamoto nyingi za udhaifu katika nyuga tofauti. Ni kwa ajili hiyo ndio maana Mutsuhito baada ya mwaka mmoja kuingia madarakani alibuni mapinduzi ya kijamii na kuanzisha marekebisho nchini Japan. Katika uwanja huo alihamisha mji mkuu kutoka Kyoto kwenya Tokyo sambamba na kubadili katiba ya nchi hiyo. Hata kama utawala wa Mutsuhito ulifikia tamati mwaka 1912, lakini Japan iliweza kupata maendeleo ingawa wakati huo huo kuliibuka vita kati ya nchi hiyo na China na Russia.

Mutsuhito

Siku kama ya leo miaka 87 iliyopita sawa na tarehe 12 Aprili 1932, mfumo wa jamhuri uliasisiwa kwa muda huko Uhispania na utawala wa kisultani ukafikia ukomo. Wananchi wa Uhispania waliokuwa wakipigania mfumo wa jamhuri waliendesha mapambano dhidi ya utawala wa kimabavu na kidikteta wa Alphonce wa 13 Mfalme wa wakati huo wa Uhispania na kumlazimisha kujiuzulu.

Bendera ya Uhispania

Na siku kama ya leo miaka 58 iliyopita, kwa mara ya kwanza mwanadamu alifika katika anga za mbali na kuizunguka dunia. Siku hiyo Yuri Gagarin mwanaanga wa Urusi ya zamani aliyekuwa na umri wa miaka 27 aliizunguka dunia kwa dakika 89 kwa kutumia chombo cha anga za mbali kwa jina la Vastok 1 na kwa msingi huo kukapatikana mafanikio makubwa katika sekta ya masuala ya anga. Gagarin alifariki dunia akiwa pamoja na mmoja wa viongozi wa ngazi za juu wa sekta ya masuala ya anga wa Urusi ya zamani katika ajali ya ndege hapo mwaka 1968.

Yuri Gagarin