Jumatatu tarehe 8 Novemba 2021
Leo ni Jumatatu tarehe Pili Rabiuthani 1443 Hijria sawa na Novemba 8 mwaka 2021.
Siku kama ya leo miaka 365 iliyopita, alizawa Edmond Halley, mtaalamu wa nyota wa nchini Uingereza. Halley alisoma katika kitengo cha Queen kilicho chini ya chuo kikuu cha Oxford, nchini humo na kuanza kujishughulisha na masuala ya utafiti wa nyota akiwa kijana mdogo, huku akifanya safari kuelekeaa kusini mwa dunia ya Bahari ya Atlantic. Edmond Halley alichukua muda mwingi katika kutalii nyota ambapo alipata kufahamu kwamba, kama ilivyo kwa sayari, nyota nazo zina mviringo na mzunguko wake maalumu. Mwaka 1704 alikuwa mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Oxford, huku akiarifishwa kuwa mtaalamu wa masuala ya nyota mwaka 1720. Halley alifariki dunia mwaka 1742 wakati akijishughulisha na masuala ya nyota.
Katika siku kama ya leo miaka 347 iliyopita, alifariki dunia John Milton, malenga wa Kiingereza. Kazi za kwanza za ushairi za John Milton zilijulikana kwa majina ya Roho na Huzuni na Roho ya Furaha. Kazi nyingine ya uandishi ya John Milton ni ile aliyoipa jina la Paradise Lost. Malenga Milton alikuwa akitetea suala la kutenganishwa serikali na kanisa, kuweko uhuru wa kuabudu na wakati huo huo aliunga mkono uchujaji wa taarifa uliokuwa ukifanywa na serikali.
Siku kama ya leo miaka 126 iliyopita sawa na tarehe 8 Novemba mwaka 1895, miale ya X iligunduliwa na Wilhem Conrad Rontgen, mwanafizikia na mwanasayansi maarufu wa Ujerumani. Mtaalamu huyo mwaka 1901 alitunukiwa tuzo ya Nobel kwa kufanikiwa kugundua miale hiyo. Kwa kuwa hakutambua miale aliyoigundua, Rontgen aliamua kuipa jina la X. Miale hiyo hupenya kwa urahisi katika mwili wa mwanadamu na kwa ajili hiyo ni njia nzuri zaidi ya kuchukua taswira ya viungo au picha ya X-ray inayotumiwa kujua sehemu za ndani ya mwili zilizodhurika au kuvunjika.
Siku kama ya leo miaka 121m iliyopita alizaliwa Bi Margaret Mitchell mwandishi wa Kimarekani huko Atlanta katika jimbo la Georgia nchini humo. Baba yake Bi Mitchell alikuwa wakili wa mahakama. Kwa muda fulani alisomea fani ya udaktari, lakini baadaye alilazimika kukatisha masomo hayo kutokana na majonzi aliyokuwa nayo kufuatia kifo cha baba yake. Margaret allianza kazi ya uandishi akiwa na miaka 22. Alizidi kupata umashuhuri baada ya kuchapisha riwaya yake aliyoiita kwa jina la "Gone with The Wind."
Na katika siku kama hii ya leo miaka 116 iliyopita aliuawa shahidi Ayatullah Ali Fumani Rashti, mwanazuoni na mpambanaji shupavu wa Iran. Alizaliwa mwaka 1268 Hijria Shamsia katika eneo la Rasht kaskazini mwa Iran na kupata elimu kwa baba yake mzazi na maulamaa wengine wa zamani hizo. Ayatullah Fumani Rashti alielekea Karbala nchini Iraq kwa ajili ya elimu ya juu akiwa na umri wa miaka 20 na kutabahari katika elimu za fiqhi, falsafa na mantiki. Mwaka 1321 Hijria alirejea katika eneo alikozaliwa la Rasht na kuanzisha harakati za kueneza maarifa ya Kiislamu. Wakati wa haharakati za ufalme wa kikatiba mwanazuoni huyo alitoa wito wa kuanzishwa utawala wa sheria za Mwenyezi Mungu nchini Iran na kukabiliwa na upinzani mkuubwa. Wapiznani wa mwanazuoni huyo hawakufurahishwa na wito huo na katika siku kama hii ya leo msomi huyo wa Kiislamu aliuawa shahidi.
