Hakika ya Uwahabi 5
Imam Ali (as) anashauri: "Tolea hoja mambo ambayo hayajatokea kwa yale ambayo tayari yametokea na tabiri matukio ambayo hayajatokea kwa kuchunguza yale ambayo tayari yamekwishatokea, maana mambo ya dunia yanafanana…”
Bismillahir Rahmanir Rahim. Tunaanza kwa jina la Mwenyezi Mungu ambaye ni mjuzi mwenye hekima anayejua yale yote yanayofichwa na kudhihiridhwa na wanadamu. Salamu za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya wale wote wanaopenda na kuvutiwa na historia; wale wanaosoma historia na kuifanyia kazi katika kubuni na kupanga mustakbali wao.
Inatutosha kufahamu umuhimu wa historia pale tunaposama na kupata ibra kutokana na maneneo ya Imam Ali (as) alipotamka kumnasihi mwanawe Imam Hassan (as) kwa kumwambia: "Ewe mwanangu! Hata kama sijaishi maisha ya waliotangulia mahala pamoja, lakini nilitupia jicho matendo yao, nikawaza habari zao na kupitia kazi (maisha) zao, ni kana kwamba nilikuwa mmoja wao, bali ni kana kwamba niliishi na wa kwanza na wa mwisho wao kutokana na yale niliyojifunza kutokana na uzoefu wa historia yao." Anashauri katika sehemu nyingine kwa kusema: “Tolea hoja mambo ambayo hayajatokea kwa yale ambayo tayari yametokea na tabiri matukio ambayo hayajatokea kwa kuchunguza yale ambayo tayari yamekwishatokea, maana mambo yote ya dunia yanafanana……”
Kwa smingi huo sisi pia katika kipindi hiki tutajaribu kutegemea vyanzo vya historia ili kuujua zaidi Uwahabi na mizizi yake ya kihistoria, karibuni.
**********
Miaka mitatu baada ya Mtume Mtukufu (saw) kuhajiri kutoka Makka kwenda Madina, Mayahudi wa Bani Nadhir, Bani Quraidhwa na Bani Qainuqah walivunja mkataba waliokuwa wameutia saini na Waislamu na kushirikiana na makafiri wa Makka kwa lemgo la kumpiga vita Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na wafuasi wake. Mtume Mtukufu (saw) alifahamu vizuri usaliti wao huo. Kufuatia vita vikali vilivyopiganwa kati ya pande mbili, Mtume aliweza kuwashinda na kuwafukuza kutoka mjini Madina. Mayahudi waliovunja mkataba na Mtume walipokuwa wanaondoka mjini Madina baadhi ya wakazi wa mji huo pia walifuatana nao. Kidhahiri watu hao walikuwa wakijifanya kuwa ni Waislamu lakini kwa hakika walikuwa na uadui na chuki kubwa dhidi ya Uislamu waliyoificha ndani ya nyoyo zao, na bila shaka Mwenyezi Mungu alifahamu vyema unafiki na chuki hiyo waliyoificha nyoyoni, na kumfahamisha Mtume wake Mtukufu (saw) pamoja na Waislamu kuhusu jambo hilo.
Anasema katika Aya ya 11 ya Suratul al-Hashr kama ifuatavyo: Huwaoni wanaofanya unafiki wanawaambia ndugu zao waliokufuru katika Watu wa Kitabu: Mkitolewa na sisi lazima tutatoka pamoja nanyi, wala hatutamtii yeyote kabisa dhidi yenu. Na mkipigwa vita lazima tutakusaidieni. Na Mwenyezi Mungu anashuhudia kuwa hao hakika bila ya shaka ni waongo.
Katika Aya hii Mwenyezi Mungu anawaarifisha wanafiki na Mayahudi kuwa ni ndugu kama ambavyo ana sema katika Aya nyingine kuwa Waislamu ni ndugu. Ni wazi kuwa udugu wa Waislamu haufungamani na ukabila, rangi wala nchi bali unafungamana na itikadi na imani yao. Kwa msingi huo udugu wa wanafiki na Mayahudi unafungamana na fikra na itikadi zao.
**************
Baadhi ya Mayahudi walipoona kwamba wana marafiki wa karibu mjini Madina walichukua uamuzi wa kuukubali Uislamu kidhahiri tu na kuishi miongoni mwa Waislamu kama Waislamu katika hali ambayo kwa hakika hawakuwa wameikubali dini hii kwa nyoyo zao. Kutokana na unafiki wao huo waliamua kueneza fikra zao potovu katika jamii ya Waislamu kwa ajili ya kupotosha dini hii tukufu ya mbinguni. Shughuli za pamoja za Mayahudi na wanafiki katika jamii ya Kiislamu taratibu zilipelekea baadhi ya Waislamu waliokuwa na imani dhaifu kukubali itikadi hizo potovu. Watu hao walijua tu dhahiri ya Qur'ani na Uislamu, na hivyo kujinyima uwezo na fursa ya kutambua kina cha maarifa yake. Walishindwa kutambua hakika na ukweli wa Aya za Qur'ani na kiburi pamoja na majivuno yao yasiyo na msingi yaliwafumba macho na kuwafanya wasiweze kudiriki wala kukiri makosa yao katika uwanja huo.
Makhawarij au wale wanaoitwa na Imam Ali (as) kuwa Mariqeen (waasi) ni miongoni mwa watu hao ambao fikra na itikadi zao potovu zilifanana sana na za Mayahudi. Mbali na fikra zao dumavu na zilizoganda, kutazama mambo kidhahiri na kuifahamu Qur'ani kijuu juu tu ni miongoni mwa mambo yanayofanana sana kati ya watu hao na Mayahudi, ambayo huwapelekea kuwatuhumu Waislamu wenzao kuwa ni Makfiri na hivyo kuhalalisha damu na mali zao. Jambo baya zaidi ni kuwa Makhawarij walihalalisha vitendo vyao vya utumiaji mabavu na kuchukulia kidhahiri na kimakosa Aya za Qur'ani, kosa ambalo kimsingi baadhi ya Mayahudi walilifanya huko nyuma kuhusiana na maneno ya Mwenyezi Mungu katika kitabu chao cha mbinguni. Mwenyezi Mungu anazungumzia katika Aya kadhaa za Qur'ani Tukufu kuhusu hiana waliyofanya Mayahudi kuhusu kitabu chao kitakatifu. Tunasoma katika Aya ya 79 ya Surat al-Baqarah kama inavyofuata: Basi ole wao wanaoandika kitabu kwa mikono yao, kisha wakasema: Hiki kimetoka kwa Mwenyezi Mungu, ili wachumie kwacho pato dogo. Basi ole wao kwa yale iliyoandika mikono yao, na ole wao kwa yale wanayoyachuma.
Tunasoma katika Aya ya 78 ya Suratu Aal Imran maneno ya Mwenyezi Mungu ambapo anaashiria moja kwa moja Mayahudi ambao wakati wa kusoma kitabu cha Mwenyezi Mungu walikuwa wakiyapotosha kwa makusudi maneno ya Muumba wao na kunasibisha Kwake uongo hali ya kuwa wanajua kuwa hayo si kweli.
*************
Baada ya Makhawarij, mtu mwingine ambaye fikra na itikadi zake zilifanana sana na za Mayahudi ni Ibn Taymiyya. Kama walivyokuwa Mayahudi, aliamini kwamba Mwenyezi Mungu ana mwili na kudai kuwa huteremka duniani kila usiku, ambapo alitaka kuthibitisha fikra yake hiyo potofu kwa kutoa mfano wa yeye kuteremka kwenye ngazi akiwa kwenye mimbar. Fikra ya kuwakufurisha Waislamu pia ilikuwa katika itikadi za Ibn Taymiyya ambapo kama walivyofanya Makhawarij alitumia kila njia kuhalalisha itikadi hiyo kutokana na kufahamu kwake kimakosa Qur'ani Tukufu. Qarne nyingi baadaye, Muhammad bin Abdul Wahhab, muasisi wa madhehebu ya Uwahabi alidhihiri na kurithi fikra hizo potovu za Ibn Taymiyya.
Katika kipindi kile cha mwanzoni mwa Uislamu ambapo Makhawarij walianza kudhihiri, Imam Ali (as) alisema kuhusiana nao: "Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu ambaye nafsi yangu iko mikononi mwake!...... Hawa watakapoondoka, watadhihiri wengine ambapo hatimaye watafuatwa na wezi wenye silaha na maharamia waporaji." Leo hii tunaona wazi utabiri huo wa Imam Ali ukiwa umethibiti mbele ya macho ya walimwengu wote. Fikra zile zile dumavu na zenye mgando, za kuchukulia mambo kidhahiri na kijuu juu, za kutumia mabavu na kuwakufurisha Waislamu zinaonekana wazi hii leo katika mawazo na tabia za Mawahabi na wafuasi wao wasiopendelea kutumia akili.
Kama walivyo Mayahudi, Mawahabi wanaamini kwamba Mwenyezi Mungu ana mwili, mikono miwili, miguu miwili, macho mawili na uso. Katika kitabu cha Mayahudi pia, Mwenyezi Mungu anachorwa humo kama kiumbe aliye na miguu miwili na kama alivyo mwanadamu, hutembea na kuteremka duniani kutoka mbinguni na kwamba ana sehemu maalumu anakoishi. Mungu wa Mayahudi hajui kila kitu, hajui mambo mengi na hata hujutia baadhi ya mambo anayoyafanya. Hushiriki mieleka na Mtume wake Ya'qoub na la kushangaza ni kuwa hatimaye hushindwa kwenye mieleka hiyo.
*****************
Kwa miaka mingi makuhani wa Kiyahudi waliandika vitabu vingi vya ufafanuzi na tafsiri walizoziandika kwa matamanio na fikra zao wenyewe na kisha kuzijumuisha katika kitabu kimoja walichokipa jina la Talmud. Kitabu hicho kinaenziwa sana na Mayahudi katika zama hizi.
Kwa mujibu wa maandishi yaliyomo kwenye kitabu hicho, roho za Mayahudi ni bora kuliko za wanadamu wengine kwa sababu kwa mujibu wa itikadi zao, roho zao ni sehemu ya Mwenyezi Mungu kama alivyo mwana kwa mzazi wake. Kwa mujibu wa imani hiyo potovu, roho za watu wasio Mayahudi ni sawa na roho za wanyama. Hivyo kama mwanadamu anavyomshinda mnyama kwa ubora Mayahudi pia ni bora kuliko wanadamu wengine. Kwa mujibu wa tafsiri zilizomo kwenye Talmud, wasio Mayahudi ni wanyama walio na miguu miwili ambao wameumbwa kwa ajili ya kuwahudumia Mayahudi. Hivyo mali na roho zao ni halali kwa ajili ya Mayahudi. Waandishi wa Talmud wanaamini kuwa hatimaye dunia na kile kilichomo vinapaswa kumilikiwa na Mayahudi, hivyo wasio Mayahudi wanapaswa kuuliwa hata kama watakuwa ni watu wema.
Kwa msingi huo, Mayahudi huhalalisha damu ya kila asiyekuwa Myahudi, na huenda huo ukawa ndio msingi wa fikra za Mawahabi kuwakufurisha Waislamu wenzao wasiokuwa wao na kuhalalisha damu na mali zao. Fikra ya utakfiri inahalalisha umwagaji wa damu ya Waislamu ambao hawafikirii kama wao. Tofauti pekee iliyopo kati ya fikra mbili hizo potofu ni kuwa Mayahudi wanalichukulia kabila kuwa kipimo cha ubora wao juu ya makabila mengine ilihali Mawahabi wanachukulia fikra na itikadi yao kuwa mizani ya kupima ubora wao juu ya Waislamu wengine na hivyo kuwapa kibali cha kuwakufurisha na kuhalalisha damu na mali zao.
Kwa kusoma Qur'ani kwa njia sahihi na kuifahamu vyema huenda tukapata kuelewa vizuri zaidi nasaha za Mwenyezi Mungu kuhusu Mayuhudi na ndugu zao wa kifikra, Mawahabi. Kwa kuzitumia vizuri nasaha hizo huenda tukafanikiwa kuzuia mauaji, uporaji, mabavu, unafiki, kujiona kuwa bora na ukufurishaji unaofanywa na Mawahabi dhidi ya Waislamu, kwa sababu kama anavyosema Imam Ali (as): Mambo ya dunia yanafanana.