-
Msemaji wa Maulamaa wa Palestina: Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yamebadilisha historia ya dunia
Feb 10, 2024 07:10Mkuu wa Baraza la Ushauri na Msemaji wa Baraza Kuu la Maulamaa wa Palestina amesema kuwa, Mapinduzi ya Kiislamu ya nchini Iran si kwa ajili ya nchi hiyo tu bali ni kwa ajili ya ulimwengu mzima kwani yamebadilisha sura ya historia ya dunia.
-
UN: Iran ina nafasi chanya katika matukio ya Asia Magharibi
Feb 10, 2024 03:53Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameelezea wasiwasi wake kuhusu hali ya mvutano inayoendelea katika eneo la Magharibi mwa Asia na kusema: Iran ina nafasi chanya katika matukio ya eneo hilo na inafanya jitihada za kuimarisha utulivu na usalama.
-
Iran yaonya kuhusu uungaji mkono wa Marekani kwa jinai za Israel
Feb 09, 2024 23:43Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameionya vikali Marekani dhidi ya kuendelea kuiunga mkono Israel na Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni, Benjamin Netanyahu.
-
Muendelezo wa juhudi za Iran katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya
Feb 09, 2024 04:44Mkuu wa Polisi wa Iran, ameeleza kuridhishwa kwake na juhudi za kitengo cha kupambana na dawa za kulevya cha kikosi hicho, na kusema jeshi hilo liangamiza watu 230 waliokuwa wahusika wakuu katika biashara haramu ya dawa za kulevya na wakati huo huo kunasa tani 500 za afyuni katika kipindi cha miezi 10 iliyopita.
-
Mwakilishi wa Iran UN: Sera ya Iran ni kutuliza hali ya mambo katika eneo
Feb 08, 2024 08:43Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesema: sera ya Iran ni kutuliza hali ya mambo katika eneo na kupunguza mivutano na mapigano.
-
Rais Raisi: Ni haki ya taifa la Iran kunufaikia na matumizi ya amani ya nishati ya nyuklia
Feb 07, 2024 23:33Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumza na mabalozi wa nchi mbalimbali waliopo hapa Tehran na kutilia mkazo wajibu wa kila taifa kufaidika na nishati ya nyuklia kwa matumizi ya amani na kwamba ni haki ya taifa la Iran pia kunufaika na nishati hiyo.
-
Msomi Mnigeria: Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni dhihirisho la kupigania uhuru duniani
Feb 07, 2024 23:33Mwanasiasa na mwandishi mashuhuri wa Nigeria amesema kuwa, Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yaliyoongozwa na Imam Khomeini (RA) ni kigezo cha wapigania uhuru kote duniani ili kuzifanya nchi zao kuwa huru.
-
Rais Raisi: Sera ya msingi ya Iran ni kuunga mkono nchi zinazojitenga na Israel
Feb 05, 2024 23:30Rais Ebrahim Raisi wa Iran amesema sera ya msingi ya Jamhuri ya Kiislamu ni kuunga mkono nchi zinazojitenga na utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Amir Abdollahian: Ni muhimu kufunguliwa tena balozi za Iran na Sudan ili kupanua ushirikiano
Feb 05, 2024 12:04Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa suala la kufunguliwa tena balozi za Iran na Sudan na kurejea shughuli za mabalozi wa nchi hizo mbili kwa ajili ya kuendeleza ushirikiano wa pande zote lina umuhimu mkubwa, na kueleza kwamba kuna matumaini ya kustawishwa zaidi ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.
-
Iran yazionya Marekani na Uingereza: Msijaribu kuzipima ghadhabu za mataifa ya eneo
Feb 05, 2024 03:16Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian amelaani vitendo vya uchokozi vya hivi karibuni dhidi ya nchi za Asia Magharibi na kuzionya Marekani na Uingereza kwamba zisijaribu kuzipima ghadhabu za mataifa ya eneo hili.