-
UNHCR: 70% ya wakimbizi wa Sudan Kusini ni watoto
Jul 18, 2016 00:13Shirika la Kuwahudumia Wakimbizi wa la Umoja wa Mataifa limeeleza wasiwasi wake juu ya ongezeko la wakimbizi wa Sudan Kusini na uhaba wa fedha za kuwahudumia wakimbizi hao; na kufichua kuwa asilimia 70 ya wakimbizi hao ni watoto wadogo.
-
IGAD yataka Sudan Kusini iwekewe vikwazo vya silaha
Jul 17, 2016 11:24Jumuiya ya Ushirikiano wa Kieneo ya Mashariki mwa Afrika IGAD imetoa mwito wa kuwekewa vikwazo vya silaha Sudan Kusini kwa shabaha ya kukomesha mapigano mapya yaliyozuka nchini humo hivi karibuni na kusababisha mauaji ya mamia ya watu.
-
FAO yatahadharisha kuhusu mgogoro wa kibinadamu Sudan Kusini
Jul 17, 2016 03:18Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) limetahadharisha kuhusu uwezekano wa kutokea mgogoro wa kibinadamu huko Sudan Kusini.
-
Jeshi la Uganda laanza kuondoa raia wake Sudan Kusini
Jul 14, 2016 11:23Msafara wa magari ya jeshi la Uganda umeingia Sudan Kusini na kuanza kuwaondoa maelfu ya raia wa nchi hiyo waliokwama mjini Juba kutokana na mapigano mapya yaliyoikumba nchi hiyo changa zaidi barani Afrika.
-
Riek Machar aondoka Juba, nchi za Ulaya zawaondoa raia wao Sudan Kusini
Jul 13, 2016 10:52Makamu wa Rais wa Sudan Kusini Riek Machar ameondoka katika mji mkuu wa nchi hiyo Juba pamoja na askari wanaomuunga mkono na kwenda kusikojulikana.
-
UNHCR: Hali ya wakimbizi Sudan Kusini ni mbaya sana
Jul 12, 2016 12:32Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) limetangaza kuwa hali ya raia wanaokimbia vita na mapigano ya ndani Sudan Kusini inatia wasiwasi mkubwa.
-
Pande hasimu nchini Sudan Kusini zatangaza usitishaji vita
Jul 12, 2016 03:17Pande mbili zinazohasimiana huko Sudan Kusini na kusababisha kuzuka upya kwa vurugu nchini humo zimetangaza kusitishwa kwa mapigano, baada ya kuwepo kwa siku kadhaa za machafuko mjini Juba zilizosababisha vifo vya mamia ya watu.
-
Raia wa Uganda wazuiwa kutembelea Sudan Kusini
Jul 11, 2016 23:16Jeshi la polisi la Uganda jana liliwapiga marufuku raia wa nchi hiyo kutembelea Sudan Kusini baada ya kuzuka mapigano mapya katika mji mkuu wa nchi hiyo Juba na kupelekea watu wasiopungua 300 kuuawa.
-
Kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Sudan Kusini
Jul 11, 2016 08:28Wanachama 15 wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wametoa taarifa wakitaka kuhitimishwa mapigano katika mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba.
-
Uganda haitatuma UPDF S/Kusini huku KQ ikisimamisha safari za ndege Juba
Jul 11, 2016 02:57Jeshi la Ulinzi la Uganda UPDF limesema halitatuma askari wake kwenda kudhibiti hali ya mambo nchini Sudan Kusini, muda mfupi baada ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuzitaka nchi za kanda ya Afrika Mashariki kuingilia kati na kusuluhisha mgogoro na mapigano mapya yaliyozuka nchini humo.