Jumuiya za kiraia Burundi zaitaka serikali kupambana na magendo ya wanawake
Jumuiya za kiraia nchini Burundi zimeitaka serikali ya nchi hiyo kukomesha magendo ya wanawake na wasichana wanaotoroshwa nchini humo na kupelekwa nchi za nje hususan Saudi Arabia.
Jumuiya za kiraia nchini Burundi zimetangaza kuwa, vitendo vya magendo ya binadamu vimeongeza nchini humo hata baada ya kugunduliwa kesi nyingi za magendo ya wasichana wanaopelekwa nchi za kigeni.
Jumuiya hizo zimetoa wito wa kuchukuliwa hatua madhubuti za kuwalinda wahanga wa magendo ya binadamu hususan wasichana na kufanyike uchunguzi wa kimataifa kuhusu suala hilo.
Siku chache zilizopita msemaji wa polisi ya Burundi alisema kuwa, hadi sasa wanawake na wasichana 267 wametoroshwa nchini Burundi na kupelekwa katika nchi za Saudi Arabia, Oman na Lebanon ambako wanafanyishwa kazi za sulubu na pengine kutumiwa vibaya kingono.