Watu kadhaa wauawa katika shambulio la Al-Shabab nchini Somalia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i10450-watu_kadhaa_wauawa_katika_shambulio_la_al_shabab_nchini_somalia
Duru za habari nchini Somalia, zimearifu kuuawa na kujeruhiwa watu kadhaa katika hujuma iliyofanywa na wanachama wa kundi la kigaidi la ash-Shabab, hii leo kusini magharibi mwa mji mkuu wa nchi hiyo, Mogadishu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 02, 2016 09:01 UTC
  • Watu kadhaa wauawa katika shambulio la Al-Shabab nchini Somalia

Duru za habari nchini Somalia, zimearifu kuuawa na kujeruhiwa watu kadhaa katika hujuma iliyofanywa na wanachama wa kundi la kigaidi la ash-Shabab, hii leo kusini magharibi mwa mji mkuu wa nchi hiyo, Mogadishu.

Abdullah Ali Watin, afisa wa ngazi za juu wa usalama nchini Somalia amesema kuwa, shambulio hilo lililotekelezwa asubuhi ya leo katika mji wa Baidoa, kilometa 250 kusini magharibi mwa mji wa Mogadishu limesababisha watu kadhaa kuuawa na wengine wengi kujeruhiwa. Mtu mmoja aliyeshuhudia hujuma hiyo amesema idadi ya wahanga wa shambulizi hilo, imeongezeka kutokana na ukubwa wa hujuma. Hii ni katika hali ambayo hapo jana Rais Hassan Sheikh Mohamoud wa Somalia aliwahutubu wabeba silaha wenye mafungamano na kundi hilo la ash-Shabab nchini humo kwamba, serikali yake itawadhaminia usalama na haki zao zote za kimsingi kukiwemo kuishi kama raia wa kawaida endapo watajisalimisha kwa hiari mbele ya maafisa usalama wa serikali. Wanachama wa kundi hilo wameshadidisha hujuma zao katika wiki za hivi karibuni nchini Somalia, ambapo makumi ya watu wameuawa katika kipindi kilicho chini ya mwezi mmoja.