Seikali ya Burundi yatuhumiwa kuwatesa wapinzani
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i10801-seikali_ya_burundi_yatuhumiwa_kuwatesa_wapinzani
Serikali ya Burundi kwa mara nyingine tena imetuhumiwa kwamba inawatesa wapinzani wake.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 08, 2016 03:00 UTC
  • Seikali ya Burundi yatuhumiwa kuwatesa wapinzani

Serikali ya Burundi kwa mara nyingine tena imetuhumiwa kwamba inawatesa wapinzani wake.

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch (HRW) limeripoti kuwa, vyombo vya upelelezi vya Burundi vinatumia sana mbinu ya mateso dhidi ya wapinzani wa serikali. Ripoti ya HRW imesema kuwa, mateso hayo yanafanyika kwa malengo ya kisiasa.

Vilevile Jeshi la Polisi na wanamgambo wa chama tawala nchini Burundi wamekuwa wakifanya ukatili na hata mauaji nchini humo hususan baada ya nchi hiyo kutumbukia katika mgogoro wa ndani zaidi ya mwaka mmoja uliopita.

Burundi ilitumbikia katika mgogoro mkubwa wa ndani Aprili mwaka jana na mauaji ya hapa na pale yamekuwa yakiripotiwa mara kwa mara nchini humo hususan baada ya Rais Pierre Nkurunziza kugombea tena kiti hicho licha ya upinzani mkubwa wa vyama vya siasa.