Baribonekeza: Burundi itakabiliana na biashara ya magendo ya binadamu
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i10837-baribonekeza_burundi_itakabiliana_na_biashara_ya_magendo_ya_binadamu
Mkuu wa Tume Huru ya Haki za Binadamu nchini Burundi amesema kuwa, nchi hiyo itakabiliana kwa nguvu zake zote za biashara ya magendo ya binadamu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 08, 2016 09:08 UTC
  • Baribonekeza: Burundi itakabiliana na biashara ya magendo ya binadamu

Mkuu wa Tume Huru ya Haki za Binadamu nchini Burundi amesema kuwa, nchi hiyo itakabiliana kwa nguvu zake zote za biashara ya magendo ya binadamu.

Jean Baptiste Baribonekeza amesema kuwa, maafisa wa vyombo vya mahakama, vyombo vya usalama na polisi ya nchi hiyo vikishirikiana na asasi za kiraia na kidini vimeazimia kung'oa mizizi ya biashara ya magendo ya binadamu nchini humo.

Mkuu wa Tume Huru ya Haki za Binadamu nchini Burundi amebainisha kwamba, tume hiyo imeweka mikakati kuhakikisha kwamba, inang'oa mizizi yote ya vitisho vinavyohusiana na magendo ya binadamu.

Wakati huo huo Pierre Nkurikiye msemaji wa jeshi la polisi nchini Burundi ametatangaza kuwa, mtandao mmoja wa magendo ya binadamu hivi karibuni uliwapeleka wasichana wadogo 267 katika nchi za Saudia Arabia, Lebanon na Oman.

Vitendo vya magendo ya binadamu vinaripotiwa nchini Burundi katika hali ambayo, nchi hiyo imeendelea kuandamwa na tuhuma za kuweko ukiukaji wa haki za binadamu nchini humo.

Ikumbukwe kuwa, Burundi ilikumbwa na mgogoro wa kisiasa kufuatia hatua ya chama tawala nchini humo CNDD-FDD kumuidhinisha Rais Pierre Nkurunziza wa nchi hiyo kugombea muhula wa tatu katika uchaguzi uliopita.