Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuacha kutumia sarafu ya dola
(last modified Sat, 08 Jun 2024 07:41:47 GMT )
Jun 08, 2024 07:41 UTC
  • Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuacha kutumia sarafu ya dola

Benki Kuu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetoa agizo la kupunguza matumizi ya dola ya Marekani katika miamala ya sasa ya bidhaa na huduma mbalimbali nchini humo.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inajaribu kupunguza utegemezi wa uchumi wa nchi hiyo kwa sarafu ya dola ya Marekani, na kuhusiana na hilo, hivi karibuni benki kuu ya nchi hiyo imetoa maagizo yenye lengo la kukabiliana na sarafu ya dola kwenye taasisi za benki na mikopo.

Benki Kuu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hivi majuzi iliamuru taasisi za mikopo na makampuni ya kifedha kuangalia upya vituo vyao vya mwisho vya malipo vya kielektroniki ili wafanye kazi na faranga za Kongo pekee.

Imeelezwa kuwa, lengo la hatua hiyo ni kukuza matumizi ya sarafu ya kitaifa na kuhimiza watu kutumia sarafu hii katika shughuli zote za sasa za bidhaa na huduma.

Katika kipindi cha muda mrefu, miamala ya dola itakuwa ghali zaidi kuliko miamala ya faranga ya Kongo, na hivyo kuhimiza wafanyabiashara na watu binafsi kuweka akaunti zao katika sarafu ya kitaifa.

 

Moja ya nyenzo kuu za Marekani kwa ajili ya kutawala uchumi wa kimataifa na kuimarisha misingi ya uongozi wa uongozi wa Washington duniani ni sarafu ya nchi hiyo ya dola, ambayo imekuwa na inaendelea kutumika mara nyingi katika vita vya kiuchumi dhidi ya nchi ambazo haziko pamoja na Marekanmi kisiasa na kimisimamo.

Serikali nyingi za ulimwengu zimefikia hitimisho hili la kimkakati kwamba ni bora kujiweka mabli na sarafu ya dola ili kupunguza athari tarajiwa na madhara yanayoweza kutokea siku zijazo na kuathiri uchumii wa nchi zao.