AU kuondoa majeshi yake Somalia mwaka 2018
Jul 19, 2016 03:10 UTC
Umoja wa Afrika (AU) umetangaza kuwa, mchakato wa kuondoa kikosi cha majeshi yake nchini Somalia (AMISOM) utaanza mwaka 2018.
Kamishna wa Amani na Usalama wa Umoja wa Afrika, Smail Chergui amekiambia kikao cha AU mjini Kigali kwamba kuondoka kwa kikosi cha AMISOM nchini Somalia kutawapa viongozi wa nchi hiyo fursa ya kusimamia wenyewe masuala ya nchi yao. Ameongeza kuwa mchakato wa kuondoa kikosi cha majeshi ya Afrika nchin Somalia (AMISOM) utaanza mwanzoni mwa mwaka 2018 na kabla ya hapo jeshi la Somalia litakuwa limeyatarishwa na kupewa mafunzo na wataalamu wa masuala ya kijeshi wa Umoja wa Afrika. Vilevile Umoja wa Afrika utashiriki katika kuratibu na kutayarisha chaguzi za Rais na Bunge nchini Somalia. Smail Chergui amesema kuwa Umoja wa Afrika pia umeanzisha mfuko maalumu wa kupambana na ugaidi barani Afrika. Somalia imekuwa katika lindi na machafuko makubwa baada ya wanachama wa kundi la kigaidi la Shabab kudhibiti maeneo mengi ya nchi hiyo mwaka 2006.Tags