Wanafunzi wa sekondari Senegal wakamatwa kwa 'ugaidi'
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i11608-wanafunzi_wa_sekondari_senegal_wakamatwa_kwa_'ugaidi'
Polisi ya Senegal inawazuilia wanafunzi wanne wa shule moja ya upili kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya kigaidi.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jul 20, 2016 07:39 UTC
  • Wanafunzi wa sekondari Senegal wakamatwa kwa 'ugaidi'

Polisi ya Senegal inawazuilia wanafunzi wanne wa shule moja ya upili kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya kigaidi.

Taarifa ya jeshi la polisi la Senegal imesema kuwa, wanafunzi hao wa sekondari wamekamatwa kwa madai ya kujihusisha na biashara ya kuwasajili vijana wenzao wajiunge na makundi ya kigaidi yaliyoko Libya na Nigeria. Maafisa wa polisi walivamia makazi ya vijana hao na kunasa majarida yenye mafundisho ya misimamo iliyofurutu ada na simu za rununu. Wanafunzi hao ambao majina yao hayajawekwa wazi walikamatwa karibu na uwanja wa ndege wa Leopold Senghor katika eneo la Yoff, viungani mwa mji mkuu Dakar. Haya yanajiri wiki mbili baada ya Rais Macky Sall wa nchi hiyo kutoa mwito kwa nchi zote duniani kushirikiana katika vita vya kupambana na ugaidi. Rais wa Senegal pia ametaka mashirika ya usalama na kijasusi ya nchi mbalimbali duniani yashirikane katika kubadilishana taarifa za kijasusi na kiusalama kuhusu vitendo vya kigaidi, kama njia ya kutia nguvu vita hivyo.