Malik Agar: Vita vya ndani Sudan huenda vikamalizika Disemba mwaka huu
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i116420-malik_agar_vita_vya_ndani_sudan_huenda_vikamalizika_disemba_mwaka_huu
Malik Agar, Makamu wa Rais wa Baraza la Utawala wa Sudan, amesema kuna uwezekano kwamba vita kati ya jeshi la serikali na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) vitamalizika kabla ya mwisho wa mwaka huu.
(last modified 2024-09-16T03:16:26+00:00 )
Sep 16, 2024 03:16 UTC
  • Malik Agar
    Malik Agar

Malik Agar, Makamu wa Rais wa Baraza la Utawala wa Sudan, amesema kuna uwezekano kwamba vita kati ya jeshi la serikali na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) vitamalizika kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Matamshi hayo yametolewa huku wataalamu wakisisitiza kuwa, jeshi la Sudan linategemea zaidi suluhisho la kijeshi kwa ajili ya kumaliza vita vyya ndani nchini humo na sio mazungumzo, baada ya kupata silaha za kisasa zaidi. 

Akihutubia mkutano wa maendeleo ya huduma za afya katika eneo la Arkuit, huko mashariki mwa Sudan, Agar amesema: "Vita vitamalizika Desemba ijayo, na mtaweza kutembea mitaani bila fimbo. Mzozo wa sasa sio vita vya kawaida, lakini ni "vita vya mamluki wasio na lengo wala itikadi vinavyosimamiwa na madola ya kikanda."

Matamshi hayo ya Makamu wa Rais wa Baraza la Utawala wa Sudan yameandamana na ongezeko kubwa la mashambulizi ya anga ya Jeshi la Sudan dhidi ya ngome za Vikosi vya Msaada wa Haraka katika majimbo ya Khartoum, Al-Jazira, Sennar na miji ya mkoa wa Darfur.

Wakati huo huo ajukwaa ya karibu na jeshi la Sudan yameripoti habari ya mauaji ya makamanda mashuhuri wa wapiganaji wa RSF.