Naibu Rais wa Kenya aliyetimuliwa adai kulikuwa na njama ya kutaka kumuuwa
(last modified Mon, 21 Oct 2024 02:49:19 GMT )
Oct 21, 2024 02:49 UTC
  • Naibu Rais wa Kenya aliyetimuliwa adai kulikuwa na njama ya kutaka kumuuwa

Naibu Rais wa Kenya aliyetimuliwa, Rigathi Gachagua amedai kujiri majaribio mawili yaliyofeli ya kutaka kumuua mwezi Agosti na Septemba mwaka huu.

Gachagua ambaye alieleza haya baada ya kuruhusiwa kutoka katika Hospitali ya Karen katika mji mkuu wa Kenya Nairobi jana Jumapili amesema kuwa majaribio hayo ya kutaka kumuuwa yalikuwa ni ya sumu katika chakula, na "aligundua" kabla ya kula chakula hicho.

Naibu Rais huyo aliyevuliwa madaraka amesema matukio hayo yalitekelezwa katika mji wa Kisumu magharibi mwa Kenya Agosti 30 na katika mji wa Nyeri katikati mwa nchi hiyo mnamo Septemba 3 mwaka huu. 

Gachagua amedai kuwa maafisa wa serikali, pamoja na idara ya intelijinsia ya kitaifa walihusika katika mpango huo.

Kimani Ichung'wah Kiongozi wa waliowengi katika Bunge la Kitaifa la Kenya amesema nadai ya Gachagua ni "ya kipubavu" na hayafai "kujibiwa.

Kimani Ichung'wah 

Mahakama Kuu nchini Kenya Ijumaa ilitoa amri ya muda ya kusimamisha kubadilishwa kwa Naibu Rais wa nchi hiyo, Rigathi Gachagua. Uamuzi huo wa Mahakama Kuu ya Kenya ulitangazwa dakika chache baada ya Bunge na Seneti kuidhinisha uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Kithure Kindiki, kama Naibu mpya wa Rais wa nchi hiyo.

 

Tags