Wananchi wa Morocco na Mauritania waandamana kulaani jinai za Israel
Wananchi wa Morocco na Mauritania wameandamana na kulaani vikali mashambulio ya utawala haramu za Israel na jinai zake dhidi ya wananchi wa Ukanda wa Gaza na Lebanon.
Maandamano hayo ni muendelezo wa maandamano mtawalia ambayo yamekuwa yakifanyika katika mataifa mbalimbai barani Afrika
Waandamanaji hao mbali na kkutangaza himaya na uungaji mkono wao kwa wananchi wa Palestina na Lebanon wamesisika wakipiga nara dhidi ya utawala haramu wa Israel pamoja na waungaji mkono wao.
Kadhalika waandamanaji hao wametoa mwito wa kupelekwa haraka misaada ya kibinadamu huko Gaza na Lebanon sambamba na kuchukuliwa hatua za kusitishwa mauaji na jinai zinazofanywa na utawala ghasibu wa Israel.
Katika majuma ya hivi karibuni, mataifa mbalimbali ya Kiafrika yakiwemo ya Morocco, Mauritania, Tunisia, Algeria na Nigeria yamekuwa yakishuhudia maandamano mara kwa mara ya kuwaunga mkono Wapalestina na Walebanon na wakati huo huo kulaani jinai na mauaji ya kimbari yanayofanywa na Israel kwa uungaji mkono kamili wa Marekani na washirika wake.