Sudan Kusini na UN zatoa chanjo ya kipindupindu huku maambukizi yakiongezeka nchini
Serikali ya Sudan Kusini, kwa ushirikiano na mashirika ya Umoja wa Mataifa imeanza kutekeleza kampeni ya utoaji chanjo ili kukabiliana na mlipuko wa kipindupindu.
Wizara ya Afya ya Sudan Kusini imeeleza kuwa wagonjwa wa kipindupindu 2,555 na vifo 32 vimeripotiwa nchini humo tangu Oktoba 28 mwaka huu huku vifo vya watoto vikiwa asilimia 37.
Watu wasiopungua 150,000 katika Kaunti ya Renky hukoi Sudan Kusini wanajiandaa kupatiwa chanjo ya kujikinga na kipindupindu ambazo zimetolewa kwa msaada wa Umoja wa Mataifa.
Wakati huo huo dozi za chanjo ya kipindupindu zaidi ya milioni moja zimepelekwa katika mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba.
Yolanda Awel Deng Waziri wa Afya wa Sudan Kusini amesema kuwa mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu hasa unawaathiri wakimbizi, watoto hasa wale walio na umri chini ya miaka mitano pamoja na wazee.