Kongo yapiga marufuku ndege kutoka Rwanda
(last modified Thu, 13 Feb 2025 02:52:28 GMT )
Feb 13, 2025 02:52 UTC
  • Kongo yapiga marufuku ndege kutoka Rwanda

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imefunga anga yake kwa ndege zote za kiraia na za serikali zilizosajiliwa au zile makazi yake nchini Rwanda.

Mamlaja husika za viwanja vya ndege vya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zimebainisha kuhusu "marufuku rasmi ya kuruka na kutua nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa ndege zote za kiraia na za serikali zilizosajiliwa nchini Rwanda au zile zilizosajiliwa kwingineko lakini makazi yake yapo  Rwanda kutokana na hali ya ukosefu wa usalama iliyosababishwa na mzozo wa kivita.

Kongo imechukua uamuzi huu ambapo juzi Jumanne mapigano yalianza tena kati ya waasi wa M23 na jeshi la Kongo katika eneo la Lubero katika jimbo la Kivu ya Kaskazini.  Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa tangu Januari 26 hadi sasa zaidi ya watu 3,000 wameuawa, 2,880 wamejeruhiwa, na wengine zaidi ya 500,000 wamelazimika kuhama makazi yao kufuatia hali ya mchafukoge inayosibu Kongo.

Wakati huo huo wanajeshi wa kulinda amani wasiopungua 20 wakiwemo 14 kutoka Afrka Kusini wameuawa katika mapigano kati ya wanamgambo wa kundi la M23 na vikosi vya serikali ya Kinshasa. Miili ya wanajeshi wa Afrika Kusini waliouawa Kongo inatazamiwa kurejeshwa nyumbani leo Alhamisi. 

Waasi wa M23  

 

Waasi wa M23 wanadai kuwa wanaudhibiti mji wa Gona na tayari wametangaza utawala wao katika mji huo.