AMISOM yapata kamanda mpya nchini Somalia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i12427-amisom_yapata_kamanda_mpya_nchini_somalia
Osman Nour Soubagleh ameteuliwa kuwa kama mpya wa askari wa Umoja wa Afrika AMISOM nchini Somalia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 02, 2016 00:12 UTC
  • AMISOM yapata kamanda mpya nchini Somalia

Osman Nour Soubagleh ameteuliwa kuwa kama mpya wa askari wa Umoja wa Afrika AMISOM nchini Somalia.

Soubagleh ameteuliwa kuwa kamanda mpya wa AMISOM katika mwendelezo wa sera za Umoja wa Mataifa za kupambana na kundi la kigaidi la ash-Shabab nchini Somalia. Afisa mmoja wa jeshi la Somalia sanjari na kuthibitisha habari hiyo amesema kuwa, operesheni za kijeshi dhidi ya wanachama wa kundi hilo zitaendelea kwa ushirikiano mkubwa ya AMISOM.

Osman Nour Soubagleh, Kamanda mpya wa operesheni za AMISOM, Somalia

Askari wa Umoja wa Afrika nchini Somalia wamepata mafanikio ya kiwango fulani ikiwa ni pamoja na kurejesha usalama katika baadhi ya maeneio ya nchi huyo, ingawa wanamgambo wa genge la ash-Shabab wamekuwa wakifanya hujuma za hapa na pale ndani ya miji tofauti ya nchi hiyo ya pembe ya Afrika. 

Wakati huo huo, Francisco Madeira, Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Afrika nchini Somalia ametangaza kuwa, tangu askari wa umoja huo walipotumwa nchini Somalia hapo mwaka 2007, wamepata mafanikio makubwa.

Madeira amesema kwa sasa Somalia inaelekea kwenye njia ya amani na utulivu.